Suzy Luhende, Shinyanga blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi amekemea vikali vitendo vya ushoga, huku akisisitiza kwamba Taasisi zinazojihusisha na mambo ya ushoga na usagaji serikali haitasita kuzichukulia hatua kari za kisheria ikiwezekana kuzifungia kabisa, kwa kuwa zinaharibu maadili ya watoto wa Shinyanga na Taifa la Tanzania kiujumla,
Agizo hilo amelitoa jana wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya Mwaka 2022/2023 kipindi cha Julai hadi Disemba Mwaka 2022 kwenye mkutano ambao umefayika katika ukumbi wa ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.
Samizi amesema kumekuwepo na mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa vijana ambao wamekuwa wakifanya mapenzi ya jinsia moja ambayo sio mira na desturi ya Kitanzania, hivyo ameitaka jamii, viongozi wa serikali, pamoja na wadau mbalimbali kushirikiana ili kutokomeza mambo hayo yasiendelee kufanyika.
"Katika mkoa wa Shinyanga mashoga wamekuwa wengi tofauti na ilivyodhaniwa, hivyo niwaombe tushirikiane kwa karibu kupambana dhidi ya mmomonyoko wa maadili kwani utasaidia kuendelea kukuza na kulinda mila na desturi na maadili mema ya Kitanzania,"amesema Samizi.
"Kutokana na wimbi kubwa la ushoga serikali itaendelea kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha inachukua hatua kali kwa taasisi zitakazo bainika kujihusisha na uhamasishaji wa mapenzi na ndoa za jinsia moja katika Wilaya ya Shinyanga ikiwezekana yafungiwe kabisa maana yanaharibu maadili ya watoto wetu,"ameongeza Samizi.
Pia amewataka viongozi wa shule kuweka mapatroni na matroni kwenye magari yanayobeba watoto,kwani kuna sehemu nyingi imeripotiwa watoto wanafanyiwa ukatili kurawitiwa ndani ya magari hayo, lakini wakiwepo hao watu matukio hayo hayatafanyika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Anord Makombe amesema serikali iendelee kuchukua hatua kali za kisheria ili kuyabaini mashirika na baadhi ya watu wanaoshawishi vijana kufanya mambo ya ushoga kufanya mambo hayo.
"Na sasa hivi maadili yameharibika sana kuanzia kwa wasanii wanacheza miziki wakiwa uchi, na wanaonyesha kwenye TV huku watoto wetu wakiangalia, hivyo tumuombe Waziri mwenye dhamana aliangalie hili, kwani tunajua wasanii ni kioo cha jamii kinaweza kuelimisha jamii, lakini imekuwa ni kuelimisha jamii kwa kuharibu maadili ya Kitanzania,amesema Makombe.
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Ally Majeshi amesema tabia hii ya ushoga haifai hata kidogo haiwezekani kufanya mapenzi mwanaume kwa mwanaume ni aibu kubwa kwa Taifa la Tanzania, hivyo amewasihi wananchi kuungana na serikali kupinga vitendo hivyo kwa sababu havifai kulingana na mira ya watanzania.
Pia Majeshi amemshauri Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Samizi kwa sababu yeye ni mwenyekiti wa kamati ya usalama ili kuondokana na ushoga aweke muda wa kufunga mabaa kwa sababu kuna maeneo wanakunywa pombe kali kuanzia mchana hadi usiku mpaka asubuhi ambapo wanakunywa wakubwa hadi watoto, hivyo mtu akilewa anaweza kufanyiwa vitendo hivyo hata bila kujijua.
"Kuna sehemu furani ya mji wa Shinyanga watu wanakunywa pombe mchana na usiku ifike sehemu watu wapewe muda wa kunywa pombe na kufunga baa, kwani wakipewa uhuru kunywa mchana mpaka asubuhi tutakemea ushoga mpaka tutaishiwa maneno na itafikia wakati watakosekana wanaume lijari na tutakosa wanaume wa kuwaowa watoto wetu wa kike, tuungane kwa pamoja kukemea ushoga na usagaji," amesema Majeshi.
Hata hivyo wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wamepokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama hicho ya mwaka 2022/2023 katika kipindi cha Julai hadi Disemba Mwaka 2022.ambapo wamewapongeza wataalamu wa manispaana kuwashauri kwamba wakati mwingine waweke mchanganuo mzuri juu ya hesabu ya fedha za mikopo asilima 10 ya vijana, walemavu na wanawake.
Pia wajumbe wameishauri Tanesco kuboresha miundombinu ya umeme na kutoa huduma iliyobora kwa wananchi, kuacha kukata kata umeme, kwani kufanya hivyo wanasababisha hasara kubwa kwa serikali na kwa wananchi ikiwepo kutokea shoti ya umeme na kusababisha vifo visivyotarajiwa.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Ally Majeshi akizungumza juu ya masuala ya ushoga na kuwataka wananchi na jamii kukemea tabia hiyo
Wajumbe wa halmashauri kuu ya Wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye mkutano wa halmashauri kuu ya wilaya
Wataalamu wa manispaa ya Shinyanga wakiendelea na mkutano baada ya kutoa ufafanuzi wa miradi mbalimbali kwe ye kikao hicho