MBUNGE WA KISHAPU BUTONDO ACHANGIA MIFUKO 100 YA SARUJI UJENZI HOSTELI YA WANAFUNZI WA KIKE SHULE YA SEKONDARI MWAMASHELE


Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mwanamke duniani mkoani Shinyanga, na kisha kuchangia Mifuko 100 ya Saruji ili kufanikisha umaliziaji ujenzi wa Hosteli ya wanafunzi wa kike Shule ya Sekondari Mwamashele wilayani Kishapu.

Na Marco Maduhu, KISHAPU

MBUNGE wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, amechangia Mifuko 100 ya Saruji ili kufanikisha ujenzi wa Hosteli katika Shule ya Sekondari ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Zoezi la uchangiaji ujenzi wa Hosteli katika Shule hiyo ya Sekondari ya Mwamashele, limefanyika jana Machi 8, 2023 kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, ambapo katika Mkoa wa Shinyanga yalifanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Akizungumza wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Hosteli ya shule hiyo Mbunge Butondo, amesema katika suala la kuboresha elimu ya mtoto wa kike, ambao wengine wanatoka umbali mrefu hivyo kwa nafasi yake kama Mbunge ataendelea kusapoti elimu, na katika kufanikisha ujenzi wa Hosteli hiyo amechangia Mifuko 100 ya Saruji.

Katika uchangiaji wa harambee ujenzi wa Hosteli katika Shule ya Sekondari Mwamashele, Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga nalo lilichangia Mifuko 45 ya Saruji, pamoja na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) ambao walitoa Mifuko 10 ya Saruji.

Aidha, kwenye harambee hiyo kilichangwa kiasi cha fedha Taslim zaidi ya Shilingi Milioni 3 ahadi Milioni 10, na mifuko ya Saruji ahadi mifuko 320.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akiwa kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake mkoani Shinyanga yaliyofanyika Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu.

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga likichangia Mifuko 45 ya Saruji ili kufanikisha ujenzi wa Hosteli ya Wasichana katika Shule ya Sekondari Mwamashele wilayani Kishapu.

Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) wakitoa Mifuko 10 ya Saruji ili kufanikisha ujenzi wa Hosteli ya Wasichana katika Shule ya Sekondari Mwamashele wilayani Kishapu.

Muonekano wa Jengo la Hosteli ya wasichana katika Shule ya Sekondari Mwamashele wilayani Kishapu.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo (kulia) akiwa kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake .

BONYEZA HAPA CHINI KUONA TUKIO ZIMA MADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE JANA WILAYANI KISHAPU
👇👇👇👇

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464