NAPOL YASHIRIKI MKUTANO WA WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU MWAKITOLYO USOMAJI MAPATO NA MATUMIZI

Mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5 wilayani Shinyanga wa kusoma mapato na matumizi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KIWANDA cha Uchenjuaji dhahabu (NAPOL ELUTION PLANT) kimeshiriki Mkutano wa Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5 wilayani Shinyanga, uliolenga kusoma mapato na matumizi.

Mkutano huo umefanyika Jumamosi Machi 11,2023 kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mwakitolyo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Shinyanga na wadau wa maendeleo.

Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5 Mathew Tune, amesema wameitisha Mkutano huo wa kusoma mapato na matumizi kwa wachimbaji kupitia umoja wao wa Vitalu, ili kutekeleza Sera ya ukweli na uwazi na kuondoa migogoro isiyo na tija ya madai ya fedha kuliwa.

“Kutosoma Mapato na matumizi huwa ni chanzo cha kutengeneza Migogoro, hivyo sisi wachimbaji wa madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 tumeamua kuweka mambo hadharani ili kuwepo na uwazi na kuondoa maneno ya kusema hela zinaliwa na viongozi,”amesema Mathew.

“Nawaomba wachimbaji wenzangu wa madini ya dhahabu tuendelee na ushirikiano ili tufikie malengo yetu na matarajio yetu hadi kufikia mwaka 2025 tunataka tuwe wachimbaji wa Kati,”ameongeza Mathew.

Naye Meneja wa Vitalu Leonard Waziri, akisoma taarifa ya uzalishaji madini kwa mwaka (2022) kupitia Vitalu vitano, amesema kwa kipindi hicho wamezalisha dhahabu gramu 18,507.8 sawa na thamani ya fedha Sh.bilioni 2.3.

Amesema kupitia uzalishaji huo wa dhahabu wameweza kulipa mapato ya Serikali kuu Sh. Milioni 165 na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Sh.milioni 7.7, huku wakichangia pia Shughuli za kijamii kwa kujenga Kituo cha Polisi, vyumba vya Madarasa kwa shule za Msingi na Sekondari na Madawati, Ofisi ya Mwenyekiti wa kijiji, Soko la Madini na kuboresha miundombinu ya uchimbaji.

Mhasibu wa umoja huo wa Vitalu Mwakitolyo Namba 5 Janeth Ngangula, akisoma taarifa ya fedha amesema kulingana na matumizi waliyoyafanya mpaka sasa kwenye Akaunti wamebakiwa na kiasi cha fedha Sh.milioni 213, na mikakati ya mwaka huu (2023) katika uchangiaji shughuli za kijamii wamepanga kununua gari la wagonjwa (Ambulance).

Aidha, Mdau wa Madini kutoka Kiwanda cha Uchenjuaji wa Madini ya dhahabu NAPOL ELUTION PLANT Meneja wa Kiwanda hicho Shaibu Juma, amepongeza viongozi wa wachimbaji Mwakitolyo namba 5 kwa kusoma mapato na matumizi na kuweka mambo yao kwa uwazi na kutoa wito kwa migodi mingine iinge utaratibu huo ambao utaondoa migogoro isiyo na tija na kusonga mbele kimaendeleo na kuongeza kasi ya uzalishaji dhahabu.

“Sisi NAPOL tupo pamoja na wachimbaji wa madini ya dhahabu na tutaendelea kuwaunga mkono ili kuhakikisha shughuli za uchimbaji madini zinaendelea vizuri na kuongeza uzalishaji wa dhahabu, na Serikali itanufaika pia kwa kupata mapato,”amesema Shaibu.

Mgeni Rasmi kwenye Mkutano huo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela, naye amewapongeza viongozi kwa maamuzi waliyoyachukua kusoma mapato na matumizi huku akitoa wito kwa viongozi wote wilayani humo kuanza ngazi ya vitongoji wajenge utaratibu wa kusomea wananchi wao mapato na matumizi kama walivyofanya Mwakitolyo namba 5.

Katika Mkutano huo ulienda sambamba na utoaji wa zawadi mbalimbali vikiwamo vyeti vya pongezi kwa Vitalu ambavyo vilifanya vizuri katika uzalishaji wa madini ya dhahabu, utoaji wa Tshet kutoka NAPOL na makabidhiano ya Tuzo kutoka Hollysmile.

Meneja wa Kiwanda cha kuchenjua Dhahabu (NAPOL ELUTION PLANT) Shaibu Juma kilichopo Kahama Mtaa wa Nyasubi akizungumza kwenye Mkutano wa Wachimbaji Wadogo wa Madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 wa usomaji mapato na matumizi.
Mwenyekiti wa CCM wilaya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela akizungumza kwenye Mkutano wa Wachimbaji Wadogo wa Madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 wa usomaji mapato na matumizi.

Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 Mathew Tune akizungumza kwenye mkutano wao wa usomaji wa mapato na matumizi.
Meneja wa Vitalu kutoka Mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 Leonard Waziri akisoma taarifa ya uzalishaji madini.

Mhasibu wa Vitalu Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 Janeth Ngangula akisoma taarifa ya mapato na matumizi.
Mdau wa maendeleo Arnold Bweichum kutoka Kampuni ya Hollysmile ya utoaji wa Tuzo Mdau Shupavu akizungumza kwenye Mkutano huo.
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.

Wadau wa madini kutoka kiwanda cha uchenjuaji wa dhahabu NAPOL Elution Plant wakiwa kwenye mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu mwakitolyo wa usomaji wa mapato na matumizi
Wadau wa madini wakiwa kwenye Mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo wa usomaji mapato na matumizi.

Wadau wa madini wakiwa kwenye Mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo wa usomaji mapato na matumizi.
Viongozi wa umoja wa Vitalu kutoka Mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomea wachimbaji mapato na matumizi.

Meneja wa Kiwanda cha uchenjuaji dhahabu (NAPOL Elution Plant) Shaibu Juma (kulia) akitoa zawadi za Tisheti kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo Namba Tano kwenye mkutano huo,(kushoto) ni Mwenyekiti wa wachimbaji Mathew Tune.

Mwenyekiti wa wachimbaji wa dhahabu Mwakitolyo namba 5 Mathew Tune akionyesha T-Sheti kutoka Kiwanda cha uchenjuaji madini ya dhahabu (NAPOL Elution Plant).

Mdau wa Maendeleo kutoka Kampuni ya Hollysmile Arnold Bweichum Mdau shupavu (kulia) akikabidhi Tuzo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5 kutokana na kuwa na mchango mkubwa Serikalini wa ulipaji mapato na kuzalisha madini kwa wingi, (kushoto) ni Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Mathew Tune.

Mdau wa Maendeleo kutoka Kampuni ya Hollysmile Arnold Bweichum Mdau shupavu (kushoto) akikabidhi Tuzo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5 kutokana na kuwa na mchango mkubwa Serikalini wa ulipaji mapato na kuzalisha madini kwa wingi, (kulia) ni Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Mathew Tune.

Tuzo ambayo wamekabidhiwa wachimbaji hao wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo namba 5.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela (kulia) akikabidhi vyeti vya pongezi wa Vitalu ambavyo vimezalisha madini kwa kiwango kikubwa.

Zoezi la utoaji vyeti vya Pongezi likiendelea kwa Vitalu ambavyo vimezalisha madini kwa kiwango kikubwa.

Zoezi la utoaji vyeti vya Pongezi likiendelea kwa Vitalu ambavyo vimezalisha madini kwa kiwango kikubwa.

Wachimbaji wado
go wa madini ya dhahabu kutoka Mgodi wa Mwakitolyo Namba 5 wakiwa kwenye Mkutano wa kusomewa mapato na matumizi.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464