Wajumbe wa kamati ya ufuatiliaji rasilimali za umma wakiwa kwenye picha ya pamoja
Suzy Luhende,Shinyanga blog
Chama cha wasioona mkoa wa Shinyanga (TLB) kimefanya ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za kilimo Mkoa wa Shinyanga na kubaini changamoto mbalimbali katika sekta hiyo zikiwemo za wakulima wadogo wadogo kutopatiwa mikopo kwa ajili ya kuboresha kilimo chao.
Hayo wameyabainisha wakati wakiwasilisha majibu ya ufuatiliaji huo ambao ulifadhiliwa na shirika la The Foundation for Civil Society, ambapo wamesema chama cha wasioona kimefanya ufuatiliaji na kubaini changamoto hizo ambazo zimekuwa zikisababisha wakulima kulima kilimo kiholela na kupata mazao machache kutokana na kutokuwa na mtaji wa kutosha na kulima kilimo kisichokuwa na tija.
Akitoa mrejesho huo mwezeshaji wa chama hicho Dickson Maganga amesema walifanya ufuatiliaji wa huduma za kilimo mkoa wa Shinyanga kwa kiasi cha Sh 43,961,224,51 milioni kilichofadhiliwa na shirika la The Foundation for Civil Society lenye makao makuu yake Dar- es -salaam walisema wamebaini changamoto za wakulima kutokuwa na elimu ya kilimo cha kisassa.

Changamoto zingine zilizoonekana ni mashamba darasa kutosimamiwa kitaalamu na maafisa kilimo na kutokuwepo kwa mashamba hayo yanayosimamiiwa na serikali,maafisa kilimo wa vijiji kutokuwa na vitendea kazi
hasa usafiri kwani wenye usafiri ni wale wa maafisa kilimo wa kata ambao hawawezi kuwafikia wananchi wote kwa wakati.
Zingine ni huduma za mbolea kuwa mbali na maeneo wanayopatikana wakulima mawakala wapo mjini, na wahitaji wa huduma hiyo wapo vijijini na wakati mwingine mahitaji hayo kutopatikana kwa mwaka mzima pia bei za mbolea kuwa juu na vitendea kazi za kilimo kuwa juu,hivyo kusababisha wakulima kulima mazao machache.
Maganga amesema katika ufuatiliaji huo walibaini mabadiliko ya tabia nchi kuwa ni changamoto kubwa katika maendeleo ya kilimo, kuendelea kutegemea mvua za msimu, baadhi ya maafisa kilimo kutowatembelea wakulima kwa ajili ya kutoa elimu ya kilimo na wakulima kutozingatia ushauri wa kitaalamu kutoka kwa maafisa kilimo, ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji wa bajeti ya kilimo kutokuwa shirikishi kwa wakulima kuanzia ngazi ya vijiji hadi kata.
"Kitu kingine ambacho tumekibaini kwa wakulima hawatumii mbolea ya kisasa wengi wao wanatumia mbolea ya asili, ambapo watu 75 kati ya 200 walioohojiwa sawa na asilimia 37 wamesema hawana elimu ya matumizi ya mbolea kutoka kwa maafisa ugani, na watu 82 sawa na asilimia 41 walisema wanatumia samadi na watu 36 sawa na asilimia 18 wanatumia mbolea ya kisasa na watu 82 sawa na asilimia 41 hawatumii kabisa"amesema Maganga.
Mwenyekiti wa mradi huo Marco Nkanjiwa amesema changamoto hizo zimesababisha wakulima wasipate mazao ya kutosha ambapo wakulima walisema ekari moja inatoa magunia tano kama yangelimwa kitaalamu wangetoa gunia 12 kwa mazao ya biashara kama pamba ekari moja inatoa kilo 4000 ambapo ingelimwa kitaalamu ingetoa kilo 7500
Katibu wa Chama Cha wasioona mkoa wa Shinyanga ambaye ndiye mratibu wa mradi huo Agnes Makambajeki amesema kamati iliyopewa elimu inatakiwa ikaelimishe wakulima walime kwa kutumia mbegu za kisasa ili waweze kuvuna mavuno mengi na kuondokana na njaa pia aliwataka wapande miti ili mvua iweze kunyesha ili ardhi iweze kupata maji na kutunza maji.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Didia na Tinde ambao wamechangia kukusanya maoni ya wakulima wamesema wakulima wengi bado hawaziamini mbolea za kisasa hivyo wengi wao wanalima hivyo hivyo bila mbolea lakini wakipewa elimu watabadilika.
Kwa upande wake afisa kilimo wa kata ya usanda Dickson Felician ambaye alikuwa amemwakilisha afisa kilimo wa halmashauri ya Shinyanga tayari serikali imetoa vitendea kazi kwa maafisa ugani wote wa Shinyanga hivyo hakutakuwa na changamoto ya maafisa ugani tena, wakulima watapewa elimu ya mbegu ili waweze kutumia na kuvuna mavuno mengi tofauti na kutumia mbegu ya samadi.
"Lakini pia wakulima wanaogopa kuitumia mbegu ya kisasa kwa kudai kuwa inaharibu ardhi, ni kweli ukianza kutumia mbolea ya kisasa lazima kila unapotaka kulima lazima utumie mbolea hiyo kwani lazima kutakuwa na mabadiliko kwa sababu itakuwa imeshazoea kupokea mbegu mpya, mbegu ya samadi yenyewe inadumu muda mrefu,amesema Felician.
Aidha kazi ya kupeleka madodoso kwenye makundi ilifanywa na kamati ya PETS iliyoundwa na wananchi wa kata husika zilizo kwenye mradi ambapo halmashauri ilikuwa na kata mbili ambayo ni Didia na Tinde na wilaya ya kahama kata nne ambazo ni Igunga, Bukomela, Kinamapula na Nyandekwa.
Mwenyekiti wa mradi huo Marco Nkanjiwa akifafanua jambo
Mwezeshaji wa chama cha wasioona Dickson Maganga akielekeza jinsi ufuatiliaji ulivyokuwa ukiendeshwa
Katibu wa Chama Cha wasioona mkoa wa Shinyanga ambaye ndiye mratibu wa mradi huo Agnes Makambajeki akifafanua jambo
Wajumbe wa kanati ya ufuatiliaji wakimsikiliza mwezeshaji
Wajumbe wa kanati ya ufuatiliaji wakimsikiliza mwezeshaji
Afisa kilimo wa kata ya usanda Dickson Felician akifafanua jambo
Mwezeshaji wa chama cha wasioona Dickson Maganga akielekeza jinsi ufuatiliaji ulivyokuwa ukiendeshwa
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464