JUMUIYA YA WAZAZI SHINYANGA YAWASHA MOTO KWA VIONGOZI NGAZI YA KATA YAAHIDI KUFANYA KAZI KWA NGUVU ZOTE



Mwenyekiti wa Jumuiya ya  wazazi CCM mkoa wa Shinyanga John Siagi akizungumza na viongozi wa Jumuiya hiyo ngazi ya kata kutoka wilaya ya Kahama ambapo aliwataka waendelee kufanya kazi kwa nguvu zote na kufundisha maadili mema kwa watoto ili kuondokana  tabia ya kufanya maovu.

 Suzy Luhende, Shinyanga Blog

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi amewataka viongozi  wa jumuiya ya wazazi kutoka kata za wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga  kufanya kazi za jumiuiya hiyo kwa nguvu zote na kuhakikisha wanayazingatia yote yale waliyofundishwa katika semina elekezi.

Licha ya kufanya kazi kwa nguvu zote pia amewataka makatibu elimu na malezi kutembelea mashuleni na kufundisha malezi na maadili mema kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, ikiwa ni pamoja na kuwataka wazazi na walezi kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao ili wasijiingize kwenye makundi mabaya yasiyo na maadili mema.

Hayo ameyasema jana wakati akizungumza na makatibu kata na makatibu elimu malezi na mazingira kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Kahama kwenye semina elekezi ya kuwajengea uwezo viongozi hao   iliyofanyika wilayani Kahama, ili waweze kufanya kazi zao kwa ufasaha zaidi, pia amesisitiza kutenga muda wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua .

"Uchaguzi umeisha sasa tunatakiwa tushirikiane,tupendane na tufanye kazi kwa nguvu zote, moto tuliouwasha katika jumuiya yetu usizimike endeleeni kufanya kazi kwa bidii zote, na mimi si mwenyekiti wa kukaa ofsini, kama  mnajambo lenu niiteeni wakati wote nipo tayari, nathamini sana jumuiya yangu, mpaka kwenye matawi mkiniarika mie nakuja wakati wowote, ili kuhakikisha jumuia inafanya kazi na kusimamia maadili ya watoto wetu"amesema Siagi.

"Sasa hivi kuna mmomonyoko wa maadili katika jamii zetu,hali ya ushoga inakuja kwa kasi imekithiri sana kwa watoto wetu wa kiume , hivyo sisi jumuia ya wazazi tusikae kusubiri viongozi wa juu kukemea tabia hii tushuke kuanzia matawi tutembelee matawi tutoe elimu ya maadili, tukifanya hivyo watoto wetu watakuwa kimbilio kwa wazazi,pia yatumieni mashirika yanayotoa elimu nzuri"ameongeza.

Aidha Siagi amewataka viongozi wa kata kuwa na miradi mbalimbali ili kuondokana na mfumo wa kuwa ombaomba, na kuhamasisha kina mama walioko vijijini na mijini ambao bado hawajajiunga na jumuia ya wazazi wajiunge wapatiwe kadi ya jumuia na ya chama, wajiunge vikundi waweze kupatiwa mikopo ya halmashauri ambayo ni asilimia nne kwa ajili ya wanawake.

Kwa upande wake katibu wa wazazi mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu akitoa elimu kwa viongozi hao amewataka viongozi wabadilike waonyesha njia, kwani mtendaji anatakiwa awe na upeo mkubwa wa kuelewa anachokifanya, aelewe wajibu wake awe na moyo wa kujitolea, aangalie malengo yake pia awe na upendo kwa watu anaowaongoza awe na hekima na uvumilivu na kuwa na hofu ya Mungu.

"Kweli wazazi tumepoteza malengo  yetu  ya malezi hatukai na kuzungumza na watoto wetu kwani wanatembea nusu uchi lakini sisi wazazi tunaangalia hatuyakemei haya,hivyo tunalaumiwa sisi wazazi tunawaachia TV wanapekechua na kuangalia vitu visivyofaa na wanaanza kujifunza wao kwa wao mwisho wanafanya kitendo  ambacho hakina maadili mema," amesema Ndulu.

"Ndio maana mvua zinakuwa za shida sana  mambo yanayofanyika kwenye jamii hayampendezi Mungu, dini zetu hazituruhusu kufanya mapenzi mwanaume kwa mwanaume na mwanamke kwa mwanamke Mungu hafurahishwi na kitendo hicho, unakuta  baba anamlawiti mwanae na anatamani kutembea na mwanae, mimba za utotoni zimekuwa nyingi mkoa wa Shinyanga tunatakiwa tutubu na tuwe na hofu ya Mungu,"amesema Rejina Ndulu.

Katibu wa Jumuia ya wazazi wilaya ya Kahama Hassan Haruna amesema jumuia ya wazazi inawajengea uwezo viongozi wake ili waweze kuwa na uelewa waweze kujisimamamia kwenye hoja mbalimbali watakazokumbana nazo ikiwa ni pamoja na kutatua migogoro mbalimbali kwa wananchi, kutoa elimu mashuleni

Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa wazazi wilaya ya Kahama Charles Lutonja amewaomba washike sana wanayofundishwa, kwani jumuia ya wazazi imekuwa ni ya muda mrefu sana, hivyo elimu watakayoivuna wakaifanyie kazi, na watendaji wanaosimamia irani ya chama cha mapinduzi CCM wakaisimamie, wakashirikiane na madiwani, watendaji wa kata na maafisa maendeleo kuhakikisha vitendo vya uovu vinatokomezwa na kuendelea kukijenga chama na jumuiya ya wazazi.

Katibu wa CCM wilaya ya Kahama  Mery Mhoha amesema mwenyekiti na katibu wanatakiwa kushirikiana,  na katibu anatakiwa atoe dira kwa viongozi wenzake anaowaongoza, na anatakiwa kuwa kioo cha jamii kuzishauri jumuia zingine, aonyeshe nidhamu kwa jumuia zote awe mbunifu na kuiongezea kipato jumuia yake.

" Kiongozi mzuri anatakiwa  asilipize kisasi asiwe mtu wa makundi, asipendelee kokote awe mtu wa kujikosoa na kukosolewa, asiwe na vitendo vya rushwa asiwe mlevi wa kubebwa asiwe mtu wa kukopa kopa kwenye nzengo awe mstari wa mbele kushiriki vikao mbalimbali vinavyomhusu vya chama na vya nzengo"amesema Mhoha.

Baadhi ya viongozi waliokuwa wakipatiwa elimu hiyo Daniel Mang"ombe na Renald Masanja wa mesema wamefurahi sana kupatiwa elimu hiyo kwani kuma vitu walikuwa hawajui, hivyo wamefundishwa na sasawatafanya kazi kwa ufasaha zaidi na kuhakikisha wanatoa elimu mashuleni ili kuhakikisha watoto wanakuwa na maadili mema.

Pia jumuia ya wazazi baada ya kumaliza kutoa elimu kwa viongozi wake pia  ilitembelea shule ya sekondari ya jumuiya ya wazazi Wigehe iliyoko wilayani Kahama ambapo ilikagua ukarabati unaoendelea katika majengo ya shule hiyo.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa Wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi akiwa na katibu wa Jumuiya hiyo mkoa wa Shinyanga  Rejina Ndulu wakiteta kitu 

Katibu wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu akiendelea kuwaelimisha viongozi wa jumuiya ya wazazi 


Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu akiwa katika ofisi ya shule ya sekondari ya Wigehe 
Mjumbe wa baraza la wazazi Taifa Edwin Nyakanyenge akizungumza na viongozi wa jumuiya ya Wazazi kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Kahama

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Kahama Mery Mhoha akizungumza na viongozi wa Jumuiya ya wazazi na kuwataka wakayafanyie kazi yale yote waliyofundishwa



Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa wazazi wilaya ya Kahama Charles Lutonja akizungumza na viongozi wa Jumuiya ya wazazi na kuwataka wakaze mwendo ili kuhakikisha jamii inakuwa na maadili mema na kuijenga Jumuia ya wazazi na Chama 


Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama Hassan Haruna akizungumza na viongozi wa Jumuiya ya wazazi ambapo aliwaomba wakakemee mimba za utotoni na wakahamasishe watoto waende shule waache utoro

Mjumbe wa baraza la wazazi Taifa Edwn Nyakanyenge akiwa na katibu elimu malezi na mazingira baada ya kukagua shule ya sekondari Wigehe iliyoko wilayani Kahama




Mjumbe wa baraza la jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga Sebastian Komaa akizungumza kwenya semina elekezi na kuwataka viongozi kuendelea kuelimisha jamii ibadilike na kuwa na maadili mema

Mwenyekiti wa Jumuiya wa wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi kushoto akiwa na mjumbe wa baraza Taifa Edwin Nyakanyenge wakiwa katika shule ya sekondari Wigehe



Mwenyekiti wa Jumuiya wa wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi akizungumza na viongozi na kuwataka wakafanye kazi huku wakimtanguliza Mungu



Mjumbe wa baraza la Jumuia ya wazazi Mkoa wa Shinyanga Agnes Kahabi akiwasalimia viongozi na kuwataka wafanye kazi kwa bidii

 wa Jumuia ya wazazi kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Kahama wakimsikiliza mwenyekiti wa Jumuiya hiyo John Siagi akiwataka waendelee kufanya kazi kwa nguvu zote Viongozi


Katibu wa Jumuia ya wazazi mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu akikagua watoto wakie delea na somo la kompyuta katika shule ya sekondari Wigehe
Viongozi wakiendelea na ukaguzi wa shule ya sekondari Wigehe 

Baada ya kukagua shule ya sekondari viongozi wa Jumuiya ya wazazi mkoa na wilaya ya Kahama 


Baada ya kumaliza ukaguzi wa shule ya Wigehe viongozi wakirudi 














Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464