Wanawake wa kata ya Mwakata halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wakisherekea siku ya wanawake duniani
Na Kareny Masasy, Msalala
KATIBU tawala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Timothy Ndanya amesema matukio ya ukatili sehemu kubwa yamewagusa wanawake hivyo ameitaka jamii kubadilika kuacha vitendo vya ubakaji na ulawiti pamoja na vipigo.
Ndanya amesema hayo leo tarehe 07/03/2023 kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani alipokuwa mgeni rasmi katika halmashauri ya Msalala yaliyofanyika kwenye kata ya Mwakata .
“Nani siku hizi anapiga mwanamke ilikuwa zamani siku hizi wanawake wanajishughulisha nakujiunga vikundi ikiwa halmashauri imekuwa ikitenga asilimia 4 mapato yake ya ndani kwaajili ya kukopesha vikundi vya wanawake vijana na watu wenye ulemavu”amesema Ndanya.
Katibu wa mpango mkakati wa kutokomeza vitendo vya ukatili kutoka halmashauri ya Msalala (MTAKUWWA)Veronica Mfuko amesema siku ya wanawake imeanza kuazimishwa mwaka 1997.
Mfumko amesema ukatili wa kimwili kwa watoto wakiume ni 96 na watoto wa kike 296 jumla yao 392 ikiwa ukatili wa kingono wanaume tisa na wasichana 15 jumla 22 ukatili wa kisaikolojia wanaume 106 na wanawake 332 jumla 438 na ,ukatili wa kiuchumi wanaume sifuri na wanawake watano.
“Wafadhili kutoka UNFPA wamejenga kituo shufaa yaani one stop centre ambapo kipo kata ya Bugarama na dawati la jinsia kituo cha Polisi Bugarama”amesema Mfuko..
Mfuko amesema watoa huduma ngazi ya jamii wamejengewa uwezo wa namna ya kuhudumia mtu aliyefanyiwa ukatili ambapo ipo changamoto ndugu kwa ndugu wanaofanyiana ukatili kumalizana kwa siri bila kuripoti masuala ya ukatili.
Ofisa maendeleo ya jamii halmashauri ya Msalala Judica Sumari amesema wanawake kutengewa siku hii lengo kupata fursa ya elimu namna ya kupambana na haki zao ambazo walikuwa wakizikosa ambapo wamekuwa wakifanya kazi kubwa nani tegemeo.
Sumari amesema wanawake ni walezi,walimu wa watoto wanahitaji kupongezwa ndiyo siku hii imepangwa ili kuelezana haki za msingi kwani walikuwa wanakosa kumiliki ardhi na watoto wa kike kutopelekwa shule.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Flora Sagasaga amesema bado jamii inaelewa baba ndiyo kiongozi wa familia hilo ni sasa lakini dunia ya sasa imebadilika wanaume wameelimika nakutoa uhuru kwa wake zao.
“Zamani mwanamke alikuwa akiogopa kujiunga kikundi kwa hofu ya kufokewa na mume wake sasa hakuna kilichobaki sisi wanawake tuwapende waume zetu na watoto ndani ya familia nakuepuka vitendo vya ukatili”amesema Sagasaga.
Wageni waalikwa wakiwa meza kuu tayari kwa maadhimisho ya siku ya wanawake yaliyofanyika kata ya Mwakata
Mgeni rasmi mkono wa kushoto ambaye ni katibu tawala wilaya ya Kahama Timothy Ndanya akiwa na diwani wa kata ya Mwakata Six Masanja
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mwakata wakijiandaa kuanza kusherehesha
Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Msalala wakifuatilia maadhimisho ya sherehe
Ofisa maendeleo wa halmashauri ya Msalala Judica Sumari akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake
Mfanyakazi wa shirika la KIWOHEDE akipokea cheti cha shukrani kutoka halmashauri ya Msalala
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Flora Sagasaga akiongea kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake
Diwani wa kata ya Mwakata Six Masanja akiongea kwenye sherehe za siku ya wanawake
Wananchi wa kata ya Mwakata wakifutilia matukio kwenye sherehe za siku ya wanawake