MWENYEKITI WAZAZI MKOA ATETA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU NA JUMUIYA ZAKE, AHAMASISHA VIKAO VYA MARA KWA MARA


mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake katika kata ya Mwendakulima wilayani Kahama


Suzy Luhende, Shinyanga

Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM na jumuia zake ngazi ya mabalozi, matawi na kata   kufanya vikao mara kwa mara ili kuboresha Chama na jumuia zake.

Hayo ameyasema jana wakati akizungumza kwenye kikao  na  wajumbe wa halmashauri kuu ngazi  ya kata  pamoja na jumuia zake na viongozi wa matawi katika kata ya Mwendakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga,ambapo pia akiwa na viongozi hao alifanikiwa kutembelea kituo cha afya cha Mwendakulima na kuwajulia hali wanawake wajawazito, wazazi na wagonjwa.

Siagi ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali wa jumuiya ya wazazi mkoa akiwemo katibu wa wazazi Rejina Ndulu na Mjumbe wa baraza la wazazi Taifa Edwin Nyakanyenge na mjumbe wa baraza mkoa Agnes Kahabi aliwasisitiza viongozi ngazi ya kata wawe wanafanya vikao mara kwa mara ili kuimalisha Chama na jumuia zake kuanzia ngazi ya mabalozi, huku wakihamasisha wananchi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

"Ndugu zangu Jumuia ya Wazazi, UWT, na Chama fanyeni vikao na kwenye vikao hivyo mtatue changamoto zilizopo kwa wananchi msiwe wavivu, kwa sababu Chama  ndio kinasimamia serikali na miradi  mbalimbali na kutetea wanyonge waweze kutendewa haki, hivyo tatueni migogoro kwa wananchi," amesema Siagi.

" Nawaomba ndugu zangu msigeuke kuwa kero kwa wananchi badala yake muwe sehemu ya kutatua kero, kwani Chama chetu ni chama cha  amani, hivyo nasisitiza ushirikiano, upendo na mshikamano, shaulianeni kwa pamoja ili kufanya vitu vizuri," amesisitiza Mwenyekiti Siagi.

Aidha Siagi ameitaka jumuia ya wazazi kupanga muda wa kutoa elimu Mashuleni na kuwasikiliza watoto ili kujua wanachangamoto gani waweze kusaidiwa, ikiwa ni pamoja na kufanya Makongamano ya kukemea ushoga ubakaji na ulawiti.

" Pia niwaombe viongozi wenzangu kwamba tunapofanya siasa tunatakiwa tuwe wabunifu wa kufanya miradi mbalimbali,  ili kuweza kujikwamua kiuchumi, kwani siasa yetu inaendana na miradi,pia wahamasisheni kina mama na vijana wachukue kadi za jumuia ya wazazi na za Chama ili waweze kujiunga vikundi wapate mikopo ya halmashauri  wafanye miradi mbalimbali ya kujiongezea kipato,"amesema Siagi.
   
Hata hivyo Siagi alifanikiwa kugawa kadi za jumuiya na chama kwa wanachama zaidi ya 50 wa kata ya Mwendakulima ambao nao waliahidi kukitumikia Chama Cha Mapinduzi kwa uaminifu wote, kwa sababu ni chama kinachojali wanyonge.

Baadhi ya wazazi, wajawazito na wagonjwa Joseph Philipo na Agnes Piter walikishukuru Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake kwa kuwakumbuka na kuwapelekea zawadi mbalimbali zikiwemo sabuni za kufulia, Mafuta ya kupaka, na Juice, ambazo zitawasaidia kwa wakati watakao kuwepo hospitalini hapo.

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu ambaye aliambatana na mwenyekiti amewataka waendelee kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha Jumuiya ya wazazi inaimarika zaidi.


Mjumbe wa baraza la Jumuiya ya wazazi Taifa Edwin Nyakanyenge akizungumza na wanachama wa kata ya Mwendakulima


Katibu wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu akizungumza na viongozi wa Chama na Jumuia zake ngazi ya kata


Diwani wa kata ya Mwendakulima akizungumza katika kikao hocho


Katibu wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa katika kituo cha afya Mwendakulima





Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi akikabidhi kadi ya Chama kwa mwananchi wa kata ya Mwendakulima


Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Shinyanga akizungumza



Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi John Siagi akitoa maelekezo kwa kaimu mganga mkuu wa kituo cha afya Mwendakulima



Mwenyekiti akitoa maelekezo katika kituo cha afya Mwendakulima




Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi akikabidhi kadi ya Chama kwa mwananchi wa kata ya Mwendakulima




Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi akimkabidhi mwanafunzi wa shule ya msingi mwenda kulima anayefanya vizuri daftari na kalamu


Katibu wazazi kata ya Mwendakulima Sophia Bujiku akimkabidhi taarifa mwenyekiti wazazi Mkoa



Katibu wa Jumuiya ya wazazi mkoa akimpongeza mwalimu wa shule ya msingi Mwendakulimakwa kupokea kadi ya Jumuia ya wazazi





Mwenyekiti wa jumuia ya Wazazi wilaya ya Kahama Charles Lutonja akimkabidhi mwanafunzi wa shule ya mdingi Mwendakulima anayefanya vizuri darasani madaftari na kalamu


Viongozi wa Jumuiya ya wazazi na Chama wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao




Viongozi mbalimbali wa kata ya Mwendakulima wakimsikiliza mwenyekiti



Mjumbe wa baraza la Jumuiya ya wazazi Taifa Edwin Nyakanyenge akizungumza na wanachama wa kata ya Mwendakulima


Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi akiwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wilaya Charles Lutonja wakipanda mti katika kituo cha afya Mwendakulima


Viongozi wa halmashauri kuu na jumuiya zake wakimsikiliza mwenyekiti akitoa maelekezo


Katibu wa Jumuia ya wazazi Mkoa Rejina Ndulu akiwa na viongozi ngazi ya kata wakipanda mti


Mwenyekiti akisalimia wagonjwa odini


Katibu akiandaa mti kwa ajili ya kuupanda



Kikao kikiendelea katika kata ya Mwendakulima



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464