SHEREHE YA WANAWAKE SHY WOMEN’S DAY OUT YAFANA, MKURUGENZI SATURA AWATAKA WAENDELEZE UMOJA WAO

Wanawake wakiburudika Sherehe ya Shy Women's Day Out na mtoa mada Dokta Kumbuka.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

SHEREHE ya wanawake Shy Women’s Day Out ambayo imeendeshwa na kikundi cha Wanawake 'Women For Change' imefanyika kwa mara sita mfululizo, huku wakitaja mafanikio makubwa ambayo wameyapata wanakikundi, ikiwemo  kusaidia jamii ambayo inaishi katika mazingira magumu pamoja na kuiunga mkono Serikali katika sekta ya elimu, Afya na kuinua uchumi.

Sherehe hizo zimefanyika Jumamosi usiku Machi 18,2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Lyakale Mjini Shinyanga huku watoa mada wakiwa ni Dokta Kumbuka, Anti Sadaka na Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura.

Akisoma Risala ya kikundi hicho cha wanawake Women’s for Change Dk. Juliety Kabengula, amesema kikundi hicho kilanzishwa mwaka 2013 na sasa kina miaka 10 na kimekuwa kikifanya Matamasha ya kukutanisha Wanawake ndani ya miaka sita mfululizo tangu mwaka 2016 hadi leo 2023.

Amesema kwenye kikundi chao ndani ya miaka hiyo 10 wameweza kuinuana kiuchumi, kusaidia Watoto na wazee ambao wanaishi katika mazingira magumu, ikiwemo kusomesha wanafunzi, kukarabati bweni katika shule ya kulea Watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija, kununua Madawati katika shule ya Solwa na Lubaga.

Amesema mbali na kuchangia maendeleo katika Sekta ya Elimu pia wamenunua mashine kwa ajili ya kusaidia Watoto Njiti ambayo hivi karibuni wataikabidhi katika hospitali ya Rufaa  ya mkoa wa Shinyanga.

“Women’s For Change tumekuwa tukiendesha Matamasha ya wanawake ndani ya miaka sita mfululizo kwa lengo la kujengeana uwezo, kujitambua, kujikwamua kiuchumi, kukabiliana na vitendo vya ukatili, pamoja na kupambania haki zetu ikiwwmo mirathi,”amesema Dk. Kabengula.

Aidha, amesema matarajio ya kikundi hicho ni kufanya uwekezaji mkubwa ili wapate kukua kiuchumi zaidi na kuendelea kuinuana wao kiuchumi pamoja na kusaidia jamii na kuungana na Serikali katika uchangiaji wa maendeleo mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura amekipongeza kikundi hicho cha Wanawake 'Women For Change' kwa kuandaa Sherehe hiyo ya wanawake, pamoja na kusaidia jamii na kushirikiana na Serikali katika mambo mbalimbali na kuwataka waendelee na umoja huo.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na kikundi hicho katika kuhakikisha wanawainua wanawake wa Manispaa ya Shinyanga kiuchumi pamoja na kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa akina mama na kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya biashara zao ikiwemo ujenzi wa masoko.

“Wanawake ni Jeshi kubwa na leo mmethibitisha hilo na kuonyesha Vita mnaiweza na Jeshi hili likitumika vizuri litachangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii na sisi Serikali tutaendelea kuwaunga mkono chini ya Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan,”amesema Satura.

Naye Mwezeshaji wa Mada ya kwanza Anti Sadaka, amewataka wanawake kujiamini, kusimama katika nafasi zao, kujipenda pamoja na kuchapa kazi kwa bidi na siyo kuwa tegemezi kwa waume zao.

Mwezeshaji Dokta Kumbuka amewataka wanawake waache pia kuishi maisha ya kuiga, pamoja na kupunguza marafiki wasiokuwa na faida (marafiki hewa) na kuacha kuchukiana bali wapendane na kushirikiana kuchapa kazi na kufanikiwa kimaendeleo.
Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akikata keki kwenye Sherehe ya Wanawake Shy Women Day Out iliyoandaliwa na kikundi cha Wanawake Women For Change.
Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akikata keki kwenye Sherehe ya Wanawake Shy Women Day Out iliyoandaliwa na kikundi cha Wanawake Women For Change.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura (kushoto) akimlisha Keki Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake Women For Change Ansila Benedict.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura (kushoto) akimlisha Keki Mwenyekiti wa Sherehe ya Shy Women's Day Out Faustina Kivambe.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye Sherehe ya Shy Women's Day Out iliyoandaliwa na kikundi cha Wanawake Women For Change.
Mwenyekiti wa kikundi cha Wanawake Women For Change Ansila Benedict akizungumza kwenye Sherehe hiyo.
Mwenyekiti wa Sherehe ya Shy Women's Day Out Faustina Kivambe akizungunza kwenye sherehe hiyo.
Dk. Juliety Kabengula, akisoma Risala ya kikundi cha Wanawake Women's For Change kwenye sherehe hiyo ya Shy Women's Day Out.
Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Sherehe hiyo ya Shy Women's Day Out.
Dokta Kumbuka akitoa Mada kwenye Sherehe ya Shy Women's Day Out.
MC Mama Sabuni mbali na kusherehesha pia alitoa ujumbe kwa wanawake kwenye sherehe hiyo.
Sherehe ya Shy Women's Day Out ikiendelea.
Wanawake wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Awali Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akiingia ukumbini.
Awali watoa Mada wakiingia ukumbini wakiwa na Mwenyekiti wa Sherehe ya Shy Women's day Out Faustina Kivambe (kulia) (kushoto) ni Anti Sadaka na (katikati) Dokta Kumbuka.
Watoa Mada wakiwa ukumbini.
Burudani zikiendelea kutolewa kwenye sherehe hiyo.
Burudani zikiendelea kutolewa kwenye sherehe hiyo.
Burudani zikiendelea kutolewa kwenye sherehe hiyo.
Burudani zikiendelea kutolewa kwenye sherehe hiyo.
Msanii Christian Bella akitoa Burudani kwenye Sherehe hiyo ya Wanawake.
Christian Bella akiendelea kutoa burudani.
Burudani zikiendelea kwenye sherehe hiyo.
Kikundi cha Wanawake Women's For Change wakiingia ukumbini.
Picha za pamoja zikipigwa na mtoa mada Dokta Kumbuka kwenye Sherehe ya Wanawake Shy Women's Day Out.
Picha ya pamoja ikipigwa kati ya kikundi cha Women For Change, Mgeni Rasmi pamoja na watoa Mada.
Picha ya pamoja ikipigwa na wanakikundi cha Women For Change na Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464