Na Shinyanga
Press Club Blog
Umoja wa
Wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM (UWT)Kata ya Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wameadhimisha siku ya wanawake
duniani kwa kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo kulawiti na ubakaji
pamoja na vipigo kwa wakina mama.
Maadhimisho
hayo yamefanyika jana March Mosi katika Kijiji cha Kidanda Kata ya Itwangi
Halmashauri ya Shinyanga ikiwa ni katika kuelekea siku ya kilele March 8,ambapo wanawake wameiomba serikali kuchukuwa hatua
kali kwa watu watakaobainika kufanya vitendo vya kulawiti watoto na ubakaji
kutokana na kuwa kinyume na maandiko ya dini na sheria ya nchi.
Akizungumza
kwenye maadhimisho hayo mgeni rasmi Mbunge wa Viti maalum (CCM)Mkoa wa
Shinyanga Santiel Kirumba amesema kuna vitendo vya ukatili vinafanyika katika
jamii lakini wanawake wengi wanashindwa kutoa taarifa na kusababisha matukio
hayo kuendelea.
Kirumba
ameitaka jamii kuvunja ukimya na kuwataja watu wanaofanya vitendo hivyo hatua
ambayo itasaidia kukomesha ukatili na kuwawezesha watoto wa kike na wa kiume
kuwa katika mazingira salama badala ya kuendelea kufumbia macho kwa kuwalinda
wahusika.
Katika hatua
nyingine Mbunge Kirumba amesikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya
wanaume kwenye familia kuwalawiti watoto
wao na wengine kuwabaka wakati kuna wanawake wengi wa umri wao ambao wanaweza
kuzungumza nao na kuwaomba watanzania kulaani vikali vitendo hivyo.
Kwa upande
wake Diwani wa Kata ya Itwangi Sonya Jilala amewataka wanaume kuacha mfumo dume
kwenye familia badala yake washirikiane na wenzi wao ili kuleta maendeleo kwani
ubabe hauna tija matokeo yake inakuwa chanzo cha ukatili ndani ya familia na
kusababisha kutengana.
Amesema wanawake wengi hawashiriki vikao vya maamuzi ngazi ya Vijiji vinapoitishwa kutokana na waume zao kuwazuia kitendo kinawanyima haki ya kupata taarifa na kujua kinachoendelea pamoja na kueleza changamoto zinazowakabili ikiwemo huduma za afya,maji na miundombinu ya barabara.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho
Baadhi ya viongozi na madiwani wakiwa kwenye maadhimisho