Mwenyekiti wa TCCIA wilayani Kahama akitoa neno mbele ya wafanyabiashara baada ya mafunzo ya usimamizi wa sheria ya kodi ya mwaka 2015.
Na
Kareny Masasy, Kahama
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa kikodi Kahama imetoa Elimu juu ya tafsiri ya Sheria ya Usimamizi wa kodi ya mwaka 2015 kwa lugha ya Kiswashili ili kuwa na urahisi wa wafanyabiashara kuzielewa na kulipa kodi kwa wakati.
Kaimu meneja kutoka mamlaka hiyo Honest Mush ambaye ni meneja msaidizi anayeshughulikia kaguzi za kodi amesema hayo jana wakati wa utoaji elimu kwa wafanyabiashara juu ya sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015.
Mushi amesema Tafsiri ya Sheria hizi Wafanyabiashara zinawahusu ambapo ameelezea kifungu 37 cha Sheria ya Usimamizi wa kodi kinachohusu uwasilishaji wa ritani ya kodi ambapo mlipaji binafsi au kampuni kukiri kuwa mwaminifu na ulipaji usio danganya au uliosahihi.
Mushi amesema kifungu cha Sheria namba 75 kinachoeleza Riba na Adhabu mbalimbali za makosa ya kikodi yatatokana na kukokotolewa kwa kosa la kufanya makadirio ya chini ya kodi halisi inayohitajika.
Mushi amesema kifungu namba 77 cha Sheria kinaeleza atakaye shindwa kutunza kumbukumbu za biashara Adhabu kwa kampuni na adhabu ya kushindwa kuwasilisha Ritani ya kodi kwa wakati ikiwa itakatwa asilimia 2.5 ya kodi iliyokadiriwa kwenye ritani.
“Nimetafsiri Sheria hizi kwa lugha ya Kiswahili ambayo itaeleweka kwa wote lengo ninataka na ninyi mzielewe kama ninavyoelewa mimi nakusiwepo ukwepaji wa kodi usio na sababu za msingi.”amesema Mushi.
Mushi amesema Malengo wamepagiwa ulipaji kodi mwaka wa fedha 2022/2023 sh Billioni 18 na tangu walivyapangiwa wamekusanya sh Billioni 10 mpaka kufikia mwezi Julai watafikisha malengo hayo.
Ofisa wa kodi kutoka TRA Godfrey Chama amesema kodi hutozwa kwa wafanyabiashara wakubwa kwa kuangalia faida ila wafanyabiashara wadogo huangalia mauzo kipindi cha Januari hadi March kila mfanyabiashara anapaswa awe amekadiriwa kodi yake.
Ofisa Elimu kwa Mlipakodi Anceth Ndailagije amesema ulipaji kodi unafuata Miongozo na Sheria ambapo kuna kukadiriwa, kukusanya,kusimamia na kuinua kiwango cha mlipakodi na kuboresha hali ya walipa kodi na kuzuia ukwepaji kodi.
Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara,viwandani na Wakulima (TCCIA) Wilayani Kahama Charles Machali alisema sheria hizo wametafsiriwa na kugawiwa na matumaini watakwenda kufanyia kazi nakulipa kodi kikamilifu.
Wafanyabiashara wilayani Kahama wakiwa kwenye mafunzo ya elimu ya mlipakodi
Wafanyabiashara wakiwa katika mafunzo juu ya elimu ya mlipa kodi
Kaimu meneja mkoa kutoka TRA mkoa wa kikodi Kahama Honest Mush ambaye ni meneja msaidizi anayeshughulikia kaguzi za kodi akitoa elimu.
Kaimu meneja mkoa kutoka TRA mkoa wa kikodi Kahama Honest Mush ambaye ni meneja msaidizi anayeshughulikia kaguzi za kodi
Mwenyekiti wa TCCIA wilaya ya Kahama Charles Machali na kaimu meneja wa TRA mkoa wa kikodi Kahama Honest Mushi wakiwa meza kuu
Afisa mlipa kodi kutoka Malmlaka ya Mapto TRA mkoa wa kikodi Kahama Godfrey Chama akitoa elimu
Wafanyakazi wa mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa kikodi Kahama wakifanya maadalizi ya utoaji elimu
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464