WANANCHI WAPATIWA ELIMU YA KILIMO CHA MBOGAMBOGA ILI KUKUZA KIPATO CHAO


  Baadhi ya wananchi waliopatiwa mafunzo ya kilimo cha mbogamboga Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye shamba la mboga na msanii Mrisho Mpoto baada ya kupatiwa mafunzo.

                                Na Shinyanga Press Club Blog

Wananchi zaidi  ya 200 wa Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga  wamepata mafunzo ya kilimo Cha kisasa cha mbogamboga na matunda,mafunzo ambayo yametolewa na Shirika la East West Seeds,TAHA kwa kushirikiana na serikali.

Mafunzo hayo yalifanyika kwenye shamba darasa lililopo Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga yakiwa na kauli mbiu hii.

" Mbegu Bora; Mapato mazuri"  kwa kuongozwa na Mashirika ya EAst West Seeds ,TAHA na serikali

Kaimu afisa  lishe wa Halmashauri ya Msalala Peter Shimba Nganzo amesema lishe bora ina umuhimu kwa   jamii katika kupambana na utapiamlo. 

"Umuhimu wa Lishe kwa wajawazito na siku elfu moja na kuanza kliniki ya wajawazito chini ya wiki 12 ili kuweza kubaini changamoto nakuzitatua mapema" amesema Nganzo.

Mgeni rasmi katika mafunzo hayo Mrisho Mpoto akiwa amefuatana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali aliwataka viongozi kuwa na Mipango endelevu ya kuwafundisha wananchi kilimo cha  kisasa.

Diwani  wa kata ya Segese  Joseph Manyala  alisema wananchi washiriki kikamilifu na kupita kukagua shamba na kujifunza ili kuleta tija na kuwezesha kukuza uchumi wao.

Washiriki wa mafunzo hayo ni kutoka Manispaa ya Kahama,Ngogwa, Wendele, Bumva, Mega, Segese,ambapo wamesema kilimo cha mbogamboga na matunda ni mkonbozi kwa wakulima



Kaimu afisa  lishe  Halmashauri ya Msalala Peter Shimba Nganzo akizungumza na washiriki wa mafunzo ya kilimo cha mbogamboga.


Washiriki wa mafunzo wakiangalia shamba la mbogamboga

           Wakiwa kwenye mafunzo

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464