Muuguzi wa Zahanati ya kijiji cha Mwakata halmashauri ya Msalala Rhobi Magambo akitoa elimu kwa mwananchi kabla ya kumpatia huduma ya chanjo ya Uviko-19.
Na
Kareny Masasy, Msalala
BAADHI ya wananchi wa kijiji cha Mwakata halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamehamasishana kuchanja chanjo ya Covid-19 katika kusherekea siku ya wanawake duniani.
Sherehe hizo kwa halmashauri hiyo imefanyika leo tarehe 07/03/2023 katika shule ya sekondari Mwakata ambapo Kabla ya kuanza sherehe hizo walihamasishwa na Afisa lishe wa halmashauri hiyo Peter Ngazo umuhimu wa chanjo hiyo ambayo ni kinga na haina madhara yoyote.
Baada ya kumaliza kutoa Elimu ya chanjo ya Covid-19 Afisa Lishe huyo aliuliza ambaye amechanja na alipochanja alipata madhara gani walijitokeza waliochanja na kueleza hakuna madhara yoyote na maisha yanaendelea.
“Tulikuwa tunadanganyana zamani kuwa ukichanja kama mjamzito mimba inatoka au ukichanja huna mimba hutapata mtoto,kama mwanaume utakosa nguvu za kiume Imani hiyo potofu tuiondoe tuchanje ili tuwe salama”amesema Ngazo.
Ngazo amesema chanjo hiyo inawahusu watu wenye umri wa kuanzia miaka 18 kwani kinga zao zinaenda zikipungua tofauti na watoto kinga zao bado ziko juu hawawezi kupata madhara ukilinganisha na mtu mzima.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mwakata Mseka Mathias amesema kuna kaya 700 ambapo wiki iliyopita kulikuwa na mkutano wa hadhara wakuhamasisha utoaji wa chanjo ya Covid-19 walijitokeza watu Zaidi ya 100 wakachanja kwa hiari yao.
Muuguzi kutoka Zahanati ya kijiji cha Mwakata Rhobi Magambo amesema wanawake ndiyo wameongoza kwa kuchanja wamehamasishana.
“Nimechanja wanawake zaidi ya 10 na mwanaume mmoja kwa haraka haraka lakini wengi wameanza kuelewa tofauti na zamani wamekuwa wakifuata wenyewe kwenye Zahanati huduma ya chanjo”amesema Magambo.
Mkazi wa kijiji cha Mwakata Helen Benjamin (52)amesema amechanja muda mrefu na hajapata madhara mwanzo alipata hofu lakini ameona hakuna kilichomtokea nakuhamasisha wengine nao wakachanja.
Muuguzi Rhobi Magambo kutoka Zahanati ya Mwakata akitoa huduma ya chanjo ya Uviko-19.Wahamasishaji wa chanjo ya Uviko -19 na utoaji elimu kutoka shirika la SHDEPHA+
Wananchi wa kata ya Mwakata wakisikiliza elimu ya Uviko-19
Ofisa lishe wa halmashauri ya Msalala Peter Ngazo akitoa elimu ya Uviko -19 kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464