Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Johari samizi akizungumza katika kongamano la mwaka la SHYEVAWC
Wadau wa kupinga ukatili kutoka mkoa wa Shinyanga na mikoa mingine wakisikiliza mada mbalimbali za ukatili.
Na mwandishi wetu.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,
Johari Samizi ametoa kauli yake juu ya hali ya ulinzi na usalama dhidi ya
vitendo vya ukatili katika wilaya ya shinyanga kwa kuagiza wazazi,sungusungu,waganga
wa jadi na asasi za kiraia na kujiepusha
na tabia ya kuendeleza vitendo vya
ukatili katika jamii.
Hayo yameelezwa na Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Bi.Johari Samizi katika Kongamano la umoja wa asasi za
kirai zinazojihusisha na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa
mkoa wa Shinyanga (Shinyanga EVAWC working Group)lilofanyika machi 9,2023
katika manispaa ya Shinyanga, ambapo asasi za kirai ishirini na nane na wadau
wengine waliweza kushiriki kwa kujadili mada mbalimbali za kutokomeza kuweza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Shinyanga Ending
violence against Women and Children working group(SHYEVAWC), waliitisha Kongamano
hilo kwa ajili ya kufanya thathimi na wadau juu ya utekelezaji wa shughuli za
mwaka 2022 katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mwenyekiti wa Shyevawc working
group, Jonathan Manyama amesema kuwa ni kundi la hiari kwa asasi za kiraia
ishirini na nane za mkoa wa Shinyanga zinatokeleza miradi ya kutokomeza ukatili
kwa mkoa wa Shinyanga.Ambapo limeundwa na maeneo manne ya uratibu,uthibiti,huduma
na mawasiliano ambapo wanachama wa kuwekwa katika makundi hayo.
“Tumeunganisha nguvu
zetu na kuweza kushirikishana ili kusaidia watoto na wanawake wa mkoa wetu,wazo
lilianza na watu sita na leo tuko ishirini na nane kwa safari hii ya miaka
miwili,Tuko hapa ili kujitathimini juu ya utekelezaji wa shughuli zetu ili
kupokea mawazo ya wengine na kupata mbinu zingine”Amesema Jonathan
“Watu wenye ubinfasi
kufikiri wanaweza wakiwa pekee yao,ila pindi wanapojikuta hawawezi ndipo wanabaki
wapweke,umoja wetu una maana zaidi na tunawakaribisha wale wote wasiotaka kukaa
pekee yao kujiunga nasi”amesema Jonathan
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,
Johari Samizi alisema ni muhumu wazazi na walezi kuhakikisha wanalea watoto wao
kwa maadili na kuwa makini na wasaidizi wa majumbani kwao na kuwapa uhuru ili
wasiweze kutumia tamaa zao za kimwili kuharibu watoto na aliwataka wazazi
kuelewa dhana ya serikali ya kutopeleka watoto wa umri mdogo wa shule za kulala moja kwa moja.
“Hatupaswi kukwepa
jukumu la kulea watoto,suala ya kuepeleka watoto wa umri wa miaka mitatu kwa
shule za kulala moja kwa moja ni ukatili kwa watoto na hata kutowapa wasaidizi
wa majumbani muda wao wa kupumzika ni ukatili pia”Amesema Johari
Aidha Johari alisema
,sungusungu ni vema wahakikishe wanatumia nguvu zao kuwafichua wabakaji na wanaowapa
mimba watoto huko pembezoni kuliko kuweka adhabu na mihemuko kwa watu wazima
wanaowafumaniwa katika maeneo yao.
Pia waganga wa jadi
wanaotoa tiba mbadala,yamkini wapo ambao hawana nia njema na huduma za afya zaidi
ya kuchochea ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni lazima ifikie hatua ya
kuwatambua vizuri.
“Kuna mitazamo wa
sungusungu kuweka nguvu nyingi juu ya adhabu na kuwatafuta watu wazima
wanaofumaniwa kuliko kuwafichua wabakaji na wale wanaowapa mimba watoto wa shule.”
Amesema Johari.
Kwa upande mwingine,Johari
alisema hataweza kuruhusu baadhi ya asasi za kiraia zinazo chochea masuala ya
ushoga katika wilaya ya Shinyanga kwani ni kinyume na maadili yetu.
“Kwa wakati wangu
,sitakubali kuona asasi inayojihusha na kuchochea ushoga inafanya kazi katika
wilaya hii,maana tunaharibu watoto wetu na hali imekuwa si nzuri kutokana na
vitendo hivyo kuendelea kwa watoto wetu kila siku”Amesema Johari.