WEADO NA WADAU WAFANYA KIKAO CHA TATHIMINI
YA MRADI WA VUNJA UKIMYA, ZUIA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI –HALMASHAURI YA WILAYA
YA SHINYANGA.
Na mwandishi wetu.
Wadau wa kutokomekeza ukatili
kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wamefanya kikao cha tathimini ya mradi
wa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni unaotekelezwa shirika la WEADO(Women Elderly Advocacy and
Development organization) katika kata za masengwa na tinde kwa ufadhili wa Foundation For Civil Society.
Kikao hicho kimefanyika leo machi
25,2023 kwa kuongozwa na Mgeni Rasmi Nuru Yunge,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri
ya wilaya ya Shinyanga aliyeambatana na Mratibu wa dawati la jinsia na watoto jeshi
la polisi Mkoa wa Shinyanga , Mrakibu mwandamzi ,Monica Sehere.Kikao hicho kimefanyika kwa
ajili ya kujadili mrejesho wa utekelezaji wa mradi wa awamu ya kwanza wa VUNJA UKIMYA,ZUIA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI
unatekelezwa kwa kipindi cha septemba,2022 hadi Aprili,2023,ambapo taarifa za
mafanikio,changamoto na matokeo yaliwasilishwa kwa wadau walioshiriki katika
mradi huo.
Kikao hicho kiliweza kuhudhuriwa
na makundi mbalimbali ikiwa maafisa maendeleo jamii,waratibu elimu kata,maafisa
ustawi,viongozi wa dini,majukwa ya wanawake, polisi kata,wazee wa mila na wakililishi
kutoka mabaraza ya watoto kutoka kata ya tinde na masengwa.
Mkurugenzi wa Shirika la WEADO,Eliasenya
Nnko ,anasema suala la kutokomeza ukatili linahitaji nguvu ya pamoja kwa ajili
ya kusaidia wanawake na watoto kwa kuwa bado mila na desturi zimekuwa ni
changamoto kwa kutoa haki kwa wanawake na watoto wa Halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga.
“Hali ya kutokomeza ukatili dhidi
ya wanawake na watoto ,inahitaji nguvu ya pamoja na tuko hapa kupeana
tathimini ya mwelekeo tulionao na kuweza kuwa na mikakati mingine kwa pamoja”Anasema
Eliasenya.
Akifungua kikao, Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Shinyanga, Nuru Yunge alisema,Halmashauri hiyo bado ina
changamoto za masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na ninashukuru
wadau wanaotekeleza miradi ili kusaidia kutokomeza ukatili katika Halmashauri yetu.
“Kikao hiki ni muhimu kwetu sote ili
tuweze kupata mazuri ambayo tuyafanyia kazi na kuweza kuweka mikakati imara ili tuweze
kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kabisa si kupunguza tu”Anasema
Nuru
Aidha,Nuru alisema Halmasahuri
hiyo inati takwa la kisheria la kutoa mikopo kwa wanawake na vijana kwa
asilimia 10 kama serikali inavyotaka na ni fursa kwa wanawake wa Halmashauri
hiyo ,Hivyo hawapaswi kuogopa.
Kwa upande wa uwasilishaji wa taarifa
za wadau waliwasilisha taarifa za mafaniko na changamoto kwa kila kundi.
Afisa Maendeleo jamii kata ya tinde
na masengwa ,walisema wanawake wamevunja ukimya na wanaweza kuripoti kwa sasa
baada ya elimu na hata kutoa huduma kwa watoto wa mazingira magumu kwa
rasilimali zao
“Wanawake wa hapa masengwa walishirikiana
kwa pamoja kutoa taarifa katika ofisi yangu kwa mwanamke aliyepigwa na mme wake”Anasema
Atupile Maseta-Afisa maendeleo kata Masengwa.
“Wanawake wanatoa maziwa na
kumtembelea mtoto anayeishi mazingira magumu” Eva E. Mlowe-Afisa maendeleo
jamii kata ya tinde.
Waratibu wa elimu kata wanasema hakuna
suala la mimba na ndoa za utotoni kwa kipindi cha desemba,2022 hadi machi,2023 kwa
kata za masengwa na tinde kwa kuwa mabaraza ya watoto yametumika kutoa elimu.
Viongozi wa dini wa kata ya tinde
na masengwa walisema,wameweka mkazo zaidi juu ya usajili wa watu we ye sifa na
vigezo vya kufunga ndoa na wametoa elimu hiyo kwa waumini.
“sheria ya dini ya uislamu
inaruhusu msichana wa miaka 14 kufungishwa ndoa,ila kwa kupitia elimu ya
WEADO,tulielimisha viongozi wa msikiti ya vitongoji na kuweka zuio la ndoa za
mikeka kwa wasichana chini ya miaka 18” Hemed Rashid-Shehe wa kata ya tinde.
“Ndani ya jumuiya zetu,tumetoa
maelezo ya vigezo Maalum vya wanaostahili umri sahihi wa kuandikisha ndoa”Esta
Eliya-Katekista –Busanda.
Upande wa jukwa la wanawake wa
kata za tinde na masengwa,walisema mradi umesaidia kuinua kiuchumi na kuwapa
ujasiri wa kujitetea juu ya haki zao.
“Nilitelekezwa na kuachiwa watoto tisa(9) na niliishi mazingira magumu ya uchumi,WEADO wamenisaidia na leo wanafundisha wanawake wenzangu kujikwamua kiuchumi”Sarah Mayunga-Katibu jukwa la wanawake tinde.
Wakilishi wa baraza la watoto
kata ya tinde na masengwa wanasema,tumefundisha wenzetu kutoa taarifa za
vitendo vya ukatili kwa waalimu na kupiga namba 116 kupitia mabaraza ya watoto.
“Watoto wameweza kubaini vitendo
vya ukatili majumbani na wana ujasiri wa kusema”Mayenga Mabula-Masengwa shule
ya msingi.
Kadhalika, Afisa wa dawati la
jinsia kituo cha polisi tinde,Norbert Boniface anasema hawajapokea kesi ya
mimba na ndoa za utotoni kwa kipinidi cha janauri hadi machi,2023 ila changamoto
ni wazazi na walezi kutokuwa na ushirikiano na jeshi la polisi.
Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Shinyanga,
Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Monica Venance Sehere,akitoa
neno kwa niaba ya jeshi la polisi ,anasema hawajapokea kesi za mimba na ndoa za
utotoni kwa kata za tinde na masengwa kwa januari hadi machi,2023 ila
changamoto kubwa ni jamii kuchelewa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi.
Katika upande mwingine,Happyness Misael, Msajili
Msaidizi wa mashirika yasiyo ya kiserikali,akitoa shukrani zake ,alisema ni
muhimu kuboresha na mfumo mzuri wa kutoa taarifa za kesi za ukatili na kujua za
mrejesho wa kesi zinazofikisha Vyombo vya dola ili kurudisha matokeo kwa jamii
ili kuweza kuisukuma kushiriki zaidi.
Joram Magana,Afisa maendeleo
jamii wilaya ya Shinyanga ,alishukuru shirika la WEADO kwa kusema wamefanikiwa
kuwa na matokeo ya kutokuwepo kwa mimba na ndoa za utotoni kwa kata hizo mbili
na kuwataka wadau wote kuweza kuwa na matokeo chanya kwa kata zingine 24 za halmshauri hiyo.
Afisa mradi wa vunja ukimya,zuia ndoa na mimba za utotoni,Winnie Hinaya akielezea kuhusu utekelezaji wa mradi.
Mratibu elimu kata ya tinde.
Mzee wa kimila na chifu Thomas Kipela kutoka kata ya tinde akizungumzia umuhimu wa kushirikisha wazee wa kimila katika afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Alfred Kasanzu mwakilish wa baraza la watoto shule ya msingi tinde akiwasilisha taarifa ya utekelezaji.
Atupokile Maseta ,Afisa maendeleo ya jamii kata ya masengwa akiwasilisha taarifa ya kata ya masengwa.
Naomi Paul Afisa ustawi jamii halmshauri ya Shinyanga akiwasilisha taarifa yake kuhusu hali ya ukatiliMipango ya utekelezaji ikiandaliwa kwa kata za tinde na masengwa.
Joram Magana afisa maendeleo wa wilaya ya shinyanga azingumza mchango wa wadau katika wilaya hiyo.