Valeria Macha kutoka Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT) akilaani tukio la ukatili la mtoto kuchomwa maji ya moto mikono yote na Baba yake mzazi, kwenye Mafunzo ya Watendaji na Mabaraza ya Kata Geita juu ya Mfumo wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora kwa kusimamia Rasilimali za nchi na utunzaji wa mazingira.
Na Marco Maduhu, GEITA
TIMU ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT) wamelaani tukio la Mtoto Elizabeth Mathias anayekadiria kuwa na miaka (9-10) ambaye anasoma darasa la Nne mkazi wa kijiji cha Nyarugusu Halmashauri ya wilaya ya Geita kwa madai ya kuiba Sh.5,000 kwa Jirani.
Akizungumzia tukio hilo leo Afisa kutoka (LEAT) Valeria Macha, amesema tukio limewasikitisha ambalo limetendwa na Baba yake mzazi na mtoto huyo kwa kumloweka mikono mwanaye ndani ya sufuria lenye maji ya moto ambalo lilikuwa jikoni.
Macha amesema, wananchi wanapaswa kupiga vita vitendo vya ukatili ambavyo vinaendelea ndani ya jamii, pamoja na kutoa taarifa kwa viongozi ili wahusika wachukuliwe hatua, na kueleza kuwa mtoto huyo tangu afanyiwe vitendo vya ukatili Aprili mosi mwaka huu, taarifa zake zilifichwa hadi jana ndipo zikatolewa na mmoja wa wasamaria baada ya kuona mtoto huyo akiteseka na vidonda.
“Huu ni ukatili wa aina gani yani baba mzazi kumchoma mtoto wake na maji tena kwa kumloweka mikono yake ndani ya sufuria ambalo lina chemka maji jikoni kisa kaiba Sh.5,000 kwa Jirani, tena pesa hiyo alimletea Baba yake huyo na akaipangia matumizi ya familia, lakini jamii kila mmoja alikuwa akiogopa kutoa taarifa za tukio hilo tubadilikeni jamani,”amesema Macha.
“Tukio hili sisi (LEAT) tulipewa taarifa na wanafunzi wetu ambao tumekuwa tukiwafundisha mafunzo ya ujawabikaji kwa jamii na utawala bora, na sisi ndiyo tukatafuta viongozi Maofisa Maendeleo na Mtendaji wa Kata husika tukaenda eneo la tukio na kumkuta mtoto akiwa na hali mbaya ikipakwa JV ndipo tukamchukua na kuja naye Hospitali ya Mkoa Geita ili apate matibabu,”ameongeza Macha.
Aidha, amewataka viongozi wa Mabaraza ya Kata, Pamoja na Watendaji wa Kata, wafuatilie taarifa za matukio ya ukatili na kuchukua hatua pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuacha kufanyia watoto vitendo vya ukatili na kuacha kuwapatia adhabu kali kupita kiasi.
Naye Mtendaji wa Kata ya Nyarugusu Lusekelo Mwaikenda, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa mtuhumiwa tayari wamemkamata na wamemfikisha Polisi.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Geita Alex Herman, amesema mtoto huyo akipona hatarudi tena kuishi na Baba yake mzazi bali watamtafutia mahali pengine pa kuishi ikiwamo kwenye nyumba za kulea watoto, sababu tayari amesha athirika kisaikolojia na pia anaishi na Mama wa Kambo ambaye hana huruma naye.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Sophia Jongo, amesema taarifa za tukio hilo bado hajazipata sababu yupo nje ya Ofisi.
Valeria Macha kutoka Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo akilaani tukio la ukatili la mtoto kuchomwa maji ya moto mikono yote na Baba yake mzazi, kwenye Mafunzo ya Watendaji na Mabaraza ya Kata Geita juu ya Mfumo wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora kwa kusimamia Rasilimali za nchi na utunzaji wa mazingira.
Valeria Macha kutoka Timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo akilaani tukio la ukatili la mtoto kuchomwa maji ya moto mikono yote na Baba yake mzazi, kwenye Mafunzo ya Watendaji na Mabaraza ya Kata Geita juu ya Mfumo wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora kwa kusimamia Rasilimali za nchi na utunzaji wa mazingira.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Geita Alex Herman, akizungumza kwenye mafunzo na kulaani tukio la mtoto kuchomwa mikono kwa maji ya moto na Baba yake, huku akiitaka jamii kupaza sauti matukio ya ukatili na kuacha kukaa kimya.
Watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Geita wakiwa kwenye mafunzo ya Uwajibikaji kwa jamii na utawala Bora pamoja na kusimamia vyema Rasilimali za nchi na utuzaji wa mazingira mafunzo ambayo yanatolewa na LEAT.
Watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Geita wakiwa kwenye mafunzo.
Mafunzo yakiendelea.
Watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Geita wakiwa kwenye mafunzo.
Watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Geita wakiwa kwenye mafunzo.
Watendaji wa Kata na Mabaraza ya Kata Geita wakiwa kwenye mafunzo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Kazi za vikundi zikiendelea.
Kazi za vikundi zikiendelea.
Kazi za vikundi zikiendelea.
Kazi za vikundi zikiendelea.
Kazi za vikundi zikiendelea.
Kazi za vikundi zikiendelea.
Kazi za vikundi zikiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464