Mhandisi Wilfred Julius Lameck akiongoza kikao kazina timu toka wizara ya maji Cha kujadili mpango wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Manispaa ya Shinyanga pamoja na miji midogo ya Tinde, Iselemaganzi na Didia kujadili kuhusu mipango ya kuboresha upatikanaji wa huduma maji kwa ubora zaidi
Na, kitendo cha mahusiano SHUWASA
Timu ya wataalam kutoka Wizara ya Maji, Taasisi mbalimbali chini ya Wizara ya Maji na Watumishi wa SHUWASA katika muendelezo wa utekelezaji wa Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga imefanya kikao kazi cha maandalizi na kujadili mipango mbalimbali ya mapitio ili kutangaza zabuni mbalimbali kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ya maji Manispaa ya Shinyanga na miji ya Didia, Iselamaganzi na Tinde
akizungumza katika kikao kazi hicho Cha kawaida na Wataalamu, Mratibu wa mradi toka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Wilfred Julius Lameck amesema kikao kazi kitafanyika kwa muda. wa siku tano kikihusisha uandaaji wa nyaraka mbalimbali za utekelezaji wa mradi.
Aidha, Mhandisi Lameck ameongeza kuwa mkataba wa ufadhili wa mradi huo wenye thamani ya Euro milioni 76 ulisainiwa toka tarehe 20.06.2022 huku utekelezaji ukiendelea kwa hatua mbalimbali na mradi huu unatarajiwa kuhudumia zaidi ya asilimia 95 ya wakaazi wa Manispaa ya Shinyanga pindi utakapokamilika
SHUWASA kupitia Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Yusuph Katopola imekuwa ikitekeleza jukumu la uboreshaji wa huduma ya upatikanaji wa maji kwa Manispaa nzima ya Shinyanga pamoja na miji midogo ya Iselemaganzi Tinde na Didia na kuhakikisha inatunza na kulinda miundombinu pamoja na vyanzo vya maji kwa ustawi wa Taifa.