Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme ,amefuturisha waumini wa dini ya kiislamu mkoani humo, na kuahidi kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini katika nyanja mbalimbali.
Mndeme akizungumza mara baada ya kumaliza kufuturisha, amewashukuru waumini wa dini ya kiislamu kwa kuhudhuria kwa wingi kujumuika pamoja, Futari ambayo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo wa madhehebu ya kikristo pamoja na watoto wenye Ualbino.
Amesema Serikali ya awamu ya sita inatambua na kuthamini mchango wa viongozi wa dini hapa nchini, ikiwamo kuombea Amani, huku akiwaomba pia wasimamie suala la Mmomonyoko wa maadili kwa vijana na kuwarudisha kwenye mstari ili taifa liendelee kubaki kuwa salama.
“Viongozi wa dini mmekuwa na mchango mkubwa sana kwa Taifa letu katika Nyanja mbalimbali ikiwamo Sekta ya Afya na Elimu, sababu Taasisi zenu mmekuwa mkimiliki shule na huduma za afya pamoja na kudumisha amani, na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia itaendelea kushirikiana na ninyi,”amesema Mndeme.
Katika hatua nyingine Mndeme amewataka wazazi mkoani humo kila mmoja atekeleze majukumu yake katika malezi, na siyo watoto kulelewa na simu na television, hali ambayo imekuwa ikisababisha kuiga mambo mabaya ambayo ni kinyume na maadili ya Mtanzania.
Naye Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya, amesema kitendo alichokifanya Mkuu huyo wa Mkoa kwa kufuturisha waumini wa dini ya kiislamu ni kikubwa, ambacho dhawabu yake atalipwa na Mwenyezi Mungu na atamzidishia zaidi ya alichotoa.
Amesema viongozi wa dini wataendelea kuliombea Amani Taifa, pamoja na kumuombea na Afya njema Mheshimiwa Rais Samia na Serikali yake yote kikiwamo na Chama cha Mapinduzi CCM, ili aendelee kuliongoza vyema Taifa na kuwaletea maendeleo Watanzania.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akizungumza kwenye hafla ya Futari kwa waumini wa dini ya kiislamu iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategile akizungumza kwenye hafla hiyo ya Futari.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye hafla hiyo ya Futari.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akionyesha Tabasamu mara baada ya kuona waumini wengi wa dini ya Kiislamu kujitokeza kushiriki kula pamoja Futari aliyoiandaa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye hafla ya kula Futari.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akichukua chakula kwa ajili ya kufuturu
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Mkusanya akifuturu.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wakifuturu.
Wauimini wa dini ya Kiislamu wakiendelea kufuturu.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Mkusanya akiwa na Mzee Alley kwenye Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Viongozi wa CCM wakiendelea kufuturu.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Clement Madinda akifuturu.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiendelea kufuturu.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiendelea kufuturu.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiendelea kufuturu.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiendelea kufuturu.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiendelea kufuturu.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiendelea kufuturu.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiendelea kufuturu.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiendelea kufuturu.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiendelea kufuturu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akifuturu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi (kushoto) akifuturu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kushoto) akiwa na Katibu wa (UWT) Mkoa wa Shinyanga wakifuturu.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiendelea kufuturu.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiendelea kufuturu.
Awali waumini wa dini ya Kiislamu wakichukua chakula kwa ajili ya kufuturu.
Awali waumini wa dini ya Kiislamu wakichukua chakula kwa ajili ya kufuturu.
Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategile awali akiongoza Swala ya saa 1 jioni kabla ya kufuturu nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiendelea na Swala kabla ya kufuturu mida ya saa 1 jioni.