NANCY FOUNDATION, SERIKALI WAMEANZA KUTEKELEZA PROGRAM YA KUONDOA WATOTO WA MITAANI MANISPAA YA SHINYANGA


Maofisa Maendeleo ya jamii, ustawi na watendaji wa Kata wakichukua taarifa za watoto wa mitaani katika Manispaa ya Shinyanga ilikujua wazazi wao na wapi wanatoka ili wapate kusaidiwa kurudishwa majumbani mwao pamoja na kuwatatulia changamoto ambazo huwakabili na kuja kuishi mitaani.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

TAASISI ya Nancy Foundation kwa kushirikiana na Serikali, wameanza kutekeleza Program ya kuondoa watoto ambao wanaishi mitaani, ili kuwarudisha kuishi na wazazi wao au walezi na kuacha kuishi katika mazingira hatarishi na kupoteza ndoto zao sababu ya kuacha kusoma shule.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Nancy Foundation Ezra Manjerenga, amesema, walifanya utafiti katika Manispaa ya Shinyanga na kuona kuna idadi kubwa ya watoto wa mitaani ambao wamekuwa wakidhurura hovyo na kuomba omba, huku wengine wakiiba mali za watu, ndipo wakaona waje na Programu ya kuwaondoa mitaani ili wakaishi na wazazi wao au walezi.

Akizungumza leo April 14, 2023 wakati wa zoezi la kuwakusanya watoto hao na kuanza kuwatambua kwa kuchukua taarifa zao, pamoja na kula nao chakula cha pamoja, amesema hakuna mtoto wa mitaani bali watoto wote wamezaliwa na wazazi wao, hivyo wazazi au walezi wanapaswa kuchukua jukumu la kuwalea na kuwapatia haki zao zote ikiwamo elimu.

“Hakuna mtoto wa mitaani kila mtoto ana wazazi wake, na watoto ni baraka na zawadi kutoka kwa mungu, kwanini leo wanaachwa hovyo mitaani, sisi tutazungumza na watoto hawa ili kuona wanakabiliwa na tatizo gani na kisha kuona namna ya kuwasaidia na kuishi kama watoto wengine na kuendelea na masomo yao,” amesema Manjerenga.

“Program hii itakwenda muda wa miezi mitatu na baada ya hapo tutaona mafanikio ambayo yamepatikana, kisha tutaendelea nayo tena hadi kuhakikisha hakuna mtoto ambaye anadhurura hovyo mitaani bali wote warudi kuishi na wazazi wao”ameongeza Majerenga.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Brandina Mwanamila eneo ambalo watoto hao hukusanyika, anasema hali ni mbaya kumekuwapo na watoto wengi wa Mtaani, na shughuli zao kubwa ni kuomba, kutumikishwa kuuza vitu mbalimbali, pamoja na kutumiwa na watu kufanya wizi wa kwenye maduka huku wengine wakifanyiwa vitendo vya ukatili ikiwamo kuingiliwa kinyume na maumbile.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, hivi karibuni ametaja takwimu za watoto wa mitaani kwa Mkoa mzima wa Shinyanga kuwa wapo 612, na jumla ya watoto ambao wanaishi katika mazingira hatarishi ni 99,939 na kutaja baadhi ya sababu zinazosababisha watoto kuishi katika mazingira hayo ni migogoro ya ndoa, umaskini, malezi duni, na uvutaji wa madawa ya kulevya.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nancy Foundation Tanzania Ezra Manjerenga akielezea program ambayo wanaiendesha ya kuondoa watoto wa mitaani katika Manispaa ya Shinyanga.
Maofisa Maendeleo ya Jamii, ustawi na watendaji wa Kata, wachikua taarifa za watoto ambao wanaishi Mitaani katika Manispaa ya Shinyanga ili kuona namna ya kuwasaidia pamoja na kuwarudisha kwa wazazi wao au walezi.
Zoezi la uchukuaji taarifa za watoto wa mitaani likiendelea.
Zoezi la uchukuaji taarifa za watoto wa mitaani likiendelea.
Zoezi la uchukuaji taarifa za watoto wa mitaani likiendelea.
Zoezi la uchukuaji taarifa za watoto wa mitaani likiendelea.
Awali Mkurugenzi wa Taasisi ya Nancy Foundation Ezra Manjerenga akila chakula cha pamoja na watoto hao wa mitaani.
Watoto wa mitaani wakila chakula ambacho kimeandaliwa na Taasisi ya Nancy Foundation.
Watoto wakiendelea kula chakula.
Watoto wakiendelea kula chakula.
Watoto wakila chakula.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464