MGODI WA ALMASI MWADUI WALIPA FIDIA WANANCHI WALIO ATHIRIKA NA TOPE LA BWAWA LA MGODI HUO


Zoezi la ulipaji Fidia wa vitu kwa waathirika wa tope bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui likifanyika.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MGODI wa Almasi Mwadui (Wiliamson Diamond LTD) umelipa Fidia wananchi ambao waliathirika na tope la bwawa la Mgodi huo, mara baada ya kupasuka kingo na kuvamia makazi yao.

Zoezi hilo la ulipaji Fidia limeendelea leo April 15, 2023 kwa Kaya 19 ambazo zilipoteza vitu vyao, huku tayari Mgodi huo ukiwa umeshalipa Fidia ya fedha kwa waathirika 294 kati ya waathirika 304 kupitia akaunti zao jumla ya fedha Sh.bilioni 1.8.

Meneja Mahusiano wa Mgodi huo Benard Mihayo, amesema kwa waathirika 10 ambao wamesalia kulipwa Fidia wana mgogoro wa kifamilia na wakimaliza kuusuluhisha watawalipa Fidia ili kila mmoja andelee na maisha yake kama zamani.

"Leo tupo kwenye zoezi la ulipaji wa Fidia ya vitu kwa waathirika ambao walipoteza vitu vyao kwa kufunikwa na Tope, na pia mwezi June tutajenga nyumba 47 kwa wananchi ambao walipoteza nyumba zao,"amesema Mihayo.

Amesema Mgodi huo utaendelea na ulipaji Fidia ili wananchi wasiishi maisha ya shida, ambapo pia kuanzia June hadi Julai watalipa tena Fidia ya mazao kwa kutoa chakula, sababu wananchi hao hawakuweza kulima kutokana na mashamba yao kufunikiwa na tope na utoaji chakula hicho utakuwa kwa awamu mbili.

Nao waathirika wa tope bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui akiwamo Mariamu Nyorobi, wamesema wanaushukuru uongozi wa Mgodi wa Mwadui pamoja na Serikali na sasa wamelipwa Fidia zao na hawakuamini na wanakwenda kuishi maisha yao kama zamani.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Grace Mwandu, ameseme zoezi la ulipwaji Fidia limekwenda vizuri, na kutoa wito kwa wananchi fedha ambazo wamelipwa Fidia wazitumie vizuri.

Aidha, Novemba mwaka jana bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui la kuhifadhia maji machafu lilipasuka kingo zake na kutiririsha tope kwenye mkazi ya watu huku vijiji viwili vikiathirika zaidi ambayo ni Ng'wanholo na Nyenzi na tayari wameshalipwa Fidia.
Meneja Mahusiano Mgodi wa Almas Mwadui Benard Mihayo (katikati) akikabidhi Fidia ya Pikipiki kwa Mwananchi ambaye alipoteza Pikipiki yake mara baada ya kufunikwa na tope la bwawa Mgodi wa Almasi Mwadui Jomu Makunza.
Muonekano wa Pikipiki.
Meneja Mahusiano Mgodi wa Almas Mwadui Benard Mihayo (kushoto) akikabidhi Fidia Jembe la kilimo kwa kutumia Ng'ombe kwa wananchi ambao waliathirika la bwawa la tope la Mgodi wa Almasi Mwadui
Meneja Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo (katikati) akikabidhi Fidia ya kitanda kwa waathirika wa tope la bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui.
Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo (kushoto) akikabidhi Fidia ya Jenereta kwa waathirika wa bwawa la tope la mgodi huo.
Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo (kushoto) akikabidhi Fidia ya Solar kwa waathirika wa bwawa la tope la mgodi huo.
Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo (kulia) akikabidhi Fidia ya Jembe kwa waathirika wa bwala la tope la mgodi huo.
Meneja Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo (kulia) akikabidhi Fidia ya chakula kwa waathirika wa tope la bwawa la mgodi huo.
Meneja Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo (kulia) akikabidhi Fidia ya chakula kwa waathirika wa tope la bwawa la mgodi huo.
Meneja Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo (kulia) akikabidhi Fidia ya Magodoro kwa waathirika wa tope la bwawa la mgodi huo.
Muonekano wa vitu ambavyo vimelipwa Fidia kwa waathiri wa tope bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui.
Muonekano wa chakula ambacho kimelipwa Fidia kwa waathirika wa tope bwawa la mgodi wa Almasi Mwadui.
Muonekano wa chakula ambacho kimelipwa Fidia kwa waathirika wa tope bwawa la mgodi wa Almasi Mwadui.
Muonekano wa vitu ambavyo vimelipwa Fidia kwa waathiri wa tope bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui.
Muonekano wa Majembe ambayo yamelipwa Fidia kwa waathirika wa tope bwawa la Mgodi wa Almas Mwadui.
Muonekano wa Magodoro ambayo yamelipwa Fidia kwa waathirika wa tope bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui.
Muonekano wa vitu ambavyo vimelipwa Fidia kwa waathiri wa tope bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui.
Muonekano wa Matorori ambayo yamelipwa Fidia kwa waathirika wa tope bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui
Muonekano wa vitu ambavyo vimelipwa Fidia kwa waathiri wa tope bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464