POLISI SHINYANGA WADAKA VITU VYA WIZI, BUNDUKI,MADAWA YA KULEVYA




Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, amebainisha hayo leo Aprili 27, 2023 wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari.

Amesema katika msako ambao wameufanya ndani ya mwezi mmoja, wamefanikiwa kukamata vitu mbalimbali vya wizi zikiwano Bunduki Tano ambazo zilikuwa zikimilikiwa kinyume na utaratibu, pamoja na madawa ya kulevya bangi kilogramu 327, kete 85, na mirungi bunda tano.

Ametaja vitu vingine ambavyo wamekamata kuwa ni madumu 16 ambayo yana mafuta ya Petrol lita 269 yakizaniwa kuibiwa katika ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR),pombe aina ya Moshi Lita 120, na viwatilifu vya Serikali ya kuuwa wadudu wa Pamba.

Ameendelea kutaja vitu vingine kuwa ni vipondozi vyenye viambata sumu ambavyo haviruhusiwi kwa matumizi ya binadamu, lita 67 za mafuta ya kula, kopyuta mbili,3 mtungi wa Gesi, vitenge doti tano, Pikipiki Sita, pamoja na vifaa vya kupiga Ramli chonganishi.

"Jeshi la Polisi kupitia kitengo chake cha upelelezi kwa kipindi hicho cha mwezi mmoja tumewafikisha mahakamani watuhumiwa 132, na kesi 62 zimefanikiwa na watuhumiwa kufungwa vifungo,"amesema Magomi.

Ametia wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, kufuata sheria za nchi wakati wote na kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu.






Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464