GAZZA FC YA FUZU KIBABE HATUA YA NUSU FAINALI KOMBE LA MUUNGANO.
Nusu Fainali ya ligi ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikihusisha timu 8 wilayani Kishapu mkoani Shinyanga imemalizika kwa GAZZA FC kuibuka kidedea kwa kuichapa TALENT 3-0. Na kufuzu kuingia katika hatua ya Fainali.
Ligi hiyo iliyoanza tarehe 23/04/2023 ikiwa na jumla ya timu nane inategemea kumalizika 26/04/2023 katika viwanja vya shule ya msingi Buduhe Wilayani Kishapu
Katika Mchezo huo, GAZZA FC walipata Mabao kupitia kwa Nyota wao Jacob Benjamin dakika 20 bao la Jummanne Tunze dakika 30 na bao la Emmanuel Izengo dakika 40
Aidha GAZZA FC imekuwa Timu ya Kwanza kufuzu kuingia hatua ya Fainali na kusubili mshindi kati ya Kishapu Veteran na Kishapu Sekondari.