Kamati ya ufatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za kilimo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya majadiliano
Suzy Luhende, Shinyanga Blog
Shinyanga.Chama cha watu wasioona mkoa wa Shinyanga (TLB) baada ya kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za kilimo na kubaini changamoto mbalimbali ikiwemo ya uhaba wa mvua, kimeishauri serikali kutengeneza vyanzo vya maji kama vile mabwawa makubwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Ushauri huo umetolewa hivi karibuni kwenye warsha ya kujadili changamoto za kilimo zilizobainika baada ya kufanya ufuatiliaji, ambapo walisema kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ni vizuri serikali ikabuni mbinu mbadala ya kuwasaidia wakulima ili waweze kujikwamua na umasikini, na ianzishe vyanzo vya maji kwa kuchimba mabwawa makubwa ambayo watakuwa wanatumia wakulima kwa ajili ya kumwagilizia mazao yao pindi mvua zinaposimama.
Luhende Masele ambaye ni diwani wa kata ya Didia amesema ili kuondokana na changamoto ya njaa inayotokana na uhaba wa mvua, pia wananchi wahimizwe kupanda miti na waifuatilie kwa kuimwagilizia, na kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, wizara ya kilimo na hali ya hewa iwe na ushirikiano wa karibu ili kuwapa taarifa mapema wakulima kwamba kuna upungufu wa mvua walime mazao ya yanayostahimili ukame.
"Unakuta mvua ilitakiwa kunyesha mwezi wa tisa lakini inakujakunyesha mwezi wa 11, hivyo mwananchi anakuwa hana taarifa yoyote lakini akipewa taarifa mapema anaweza akajipanga vizuri kwa ajili ya kilimo, hivyo ni vizuri taasisi za serikali wizara na idara ya kilimo wakakaa pamoja ili kujua mvua zinanyesha lini,"amesema Masele.
Mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu mkoa wa Shinyanga Richard Mpongo amesema kilimo cha umwagiliaji katika mkoa wa Shinyanga ni cha muhimu sana na kinahitaji uwekezaji mkubwa, hivyo yakitengenezwa mabwawa makubwa na wananchi wakapewa elimu itamkomboa mkulima ambaye ataweza kulima kwa kilimo cha umwagiliaji.
Kwa upande wake afisa kilimo wa kata ya usanda Dickson Felician ambaye alikuwa amemwakilisha afisa kilimo wa halmashauri ya Shinyanga,amesema serikali iliyopo madarakani inathamini kilimo, hivyo hakuna kinachoshindikana na kilio hiki kikimfikia Rais uwezekano wa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji kinawezekana.
Afisa Dawati la uzuiaji Rushwa Takukuru mkoa wa Shinyanga Reuben Chongolo amesema sera ya kilimo itekeleze kwa vitendo na ili mkulima aweze kulima kilimo cha umwagiliaji kuliko kutegemea mvua ambayo wakati mwingine inachelewa kunyesha wakati mwingine inawahi ,ikiwa ni pamoja na kuwepo na usimamizi mzuri wa dawa za ruzukuku,na kuna maeneo dawa ya viuatilifu haikuuwa wadudu, kama ni elimu itolewe kwa wakulima wajue wanakosea wapi.
Pia anesema serikali itenge maeneo ya wafugaji na wakulima na kila mmoja akae kwenye eneo lake ili kuondokana na migogoro mbalimbali, na uwepo usimamizi mzuri wa ardhi wasiingiliane wafugaji na wakulima kwa sababu mifugo inaharibu mazao ya wakulima.
Diwani viti maalumu ambaye pia ni mkulima Helena Daudi amesema pembejeo zote za kilimo zinatakiwa zipatikane kuanzia mwezi wa saba katika mwaka wa fedha na zipelekwe kwenye kata husika au vijiji na usajili uwe endelevu na gharama za pembejeo mbalimbali ziwekewe ruzuku, pamoja na serikali iendelee kuwasaidia wakulima.
Mwezeshaji wa chama hicho Dickson Maganga amesema vyama vya ushirika viimarishwe viwe imara ili ruzuku ziwe zinapita kwenye vyama hivyo, na viweze kuwahudumia wakulima na serikali iunde vyombo vya kusimamia mazao ya biashara ili mkulima asipunjike aweze kupata bei nzuri, na zitungwe sheria ndogo ndogo za kilomo kwa wasiolima wavivu wanaopenda kucheza bao na kutembea mitaani tu,
Kwa upande wake mwenyekiti wa mradi huo Marco Nkanjiwa, amesema mradi huo umelenga kubolesha kilimo na kuihamasisha sera ya kilimo iweze kutekeleza sera yake kwa vitendo, kwani kila mkulima akiboreshewa na akaweza kupata vyanzo vya maji kwa ajili ya umwagiliaji na wakukima wakapatiwa ruzuku kwa wakati mkulima atajikomboa hakutakuwepo na balaa la njaa
Diwani wa kata ya Didia Jafari Kanora ambaye alikuwa mwenyekiti wa muda kwenye majadiliano hayo amesema ili kukabiliana na tabia nchi wananchi wanatakiwa kupanda miti na kuacha kukatakata miti ili mvua ziendelee kunyesha
Mwenyekiti wa mradi huo Marco Nkanjiwa, akizungumza na wajumbe
Diwani wa kata ya Didia Luhende Masele akichangia jambo
Diwani wa kata ya Tinde Jafari Kanora akifafanua jambo
Afisa Dawati la uzuiaji Rushwa Takukuru mkoa wa Shinyanga Reuben Chongolo akitoa elimu inayohusu masuala ya rushwa kwenye kikao hicho
afisa kilimo wa kata ya usanda Dickson Felician ambaye alikuwa amemwakilisha afisa kilimo wa halmashauri ya Shinyanga,alitoa maelekezo kwenye majadiliano hayo
Mjumbe wa kamati ya ufatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za kilimo
Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu mkoa wa Shinyanga Richard Mpongo akiwa kwenye kikao cha majadiliano
Wajumbe wakiendelea na majadiliano

Diwani viti maalumu Shinyanga Helena Daudi akiwa kwenye kikao hicho
Kazi ikiendelea
Wajumbe wakiendelea na majadiliano
Mwenyekiti wa mradi huo Marco Nkanjiwa, akiendelea kuelimisha kamati ya ufuatiliaji masuala ya kilimo
Wajumbe wakiwa kwenye majadiliano