KANISA LA WASABATO LAFUTURISHA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU SHINYANGA, WATOA ZAWADI YA EID

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya (kulia) Vitabu vya ‘Jipatie Amani ya Moyo’ 
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu (Nyanza Gold Belt) limewafuturisha Waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni Mwendelezo wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo viongozi wote wa dini wametumia fursa hiyo kuiombea nchi ya Tanzania amani, utulivu na mshikamano pamoja na kuombea viongozi wa taifa wakiongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hafla hiyo ya Futari iliyoandaliwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando imefanyika leo Jumanne Aprili 18, 2023 katika Hoteli ya Karena Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando ametumia fursa hiyo pia kukabidhi zawadi ya Mbuzi na Mchele kwa ajili ya Eid kwa Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya pamoja na Vitabu vya ‘Jipatie Amani ya Moyo’ kwa Sheikh Makusanya na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.

Akizungumza wakati wa Iftar hiyo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando amesema Kanisa la Waadventista Wasabato linaamini juu ya mahusiano baina yao na wenzao walio katika dini mbalimbali, madhehebu mbalimbali ya Kikristo lakini pia linaamini katika mahusiano na hata wale wasiomjua Mungu kwa sababu ni binadamu wenzao.

 "Kwa hiyo kwa muktadha huo kwa kutambua kwamba wenzetu, ndugu zetu Waislamu wamekuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na sisi tunafurahishwa sana kwa kuona kujitoa kwao katika kumtafuta Mwenyezi Mungu ndani ya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani ikizingatiwa kuwa wamekuwa wakikisisitiza umoja nasi tunafurahishwa na hilo",amesema Askofu Sando.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akizungumza wakati wa Hafla ya Futari.

"Mwezi huu Waislamu wanaamini kuwa mioyo yao katika Mwezi huu inachipuka upya na baada ya hapa wanaenda kuendeleza maisha ya uadilifu katika jamii na kwa sababu hiyo kwa sababu kanisa la Waadventista Wasabato tunaamini katika hayo ambayo Waislamu wanayaamini tukaona basi ni vyema katika kipindi hiki tuandae Iftar hii iwe ni sehemu ya kusema nyinyi ni ndugu zetu lakini iwe sehemu ya kuungana nanyi kumuomba Mwenyezi Mungu ili aweze kutupa amani katika maisha yetu, jamii zetu, taifa letu la Tanzania na kuomba Mwenyezi Mungu amjaalie Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi mbalimbali wa nchi hii amani ya bwana itawale. Tutakiane heri, Baraka za bwana ziwe juu yetu",amesema Askofu Sando.

Askofu huyo amesema Kanisa la Waadventista Wasabato linaungana na Waislamu na ameomba wawe kitu kimoja kulaani kabisa vitendo viovu vinavyoendelea katika ulimwengu hasa vitendo vya Ushoga na Usagaji na vitendo vingine ya ukatili yakiwemo mauaji ili kuwa na jamii na taifa lenye amani.

Kwa Upande wake Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya amelipongeza na kulishukuru Kanisa la Waadventisa Wasabato kwa kuandaa Futari hiyo akisisitiza kuwa hilo ni jambo la heri na wasisite kuandaa tena.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu.

“Sisi ni ndugu wa damu moja, hivyo leo ndugu wamefuturishana. Jambo hili la sisi Waislamu kukaribishwa na ndugu zetu kwa ajili ya chakula ni jambo adhimu sana. Naomba jambo hili ambalo limehudhuriwa pia na viongozi wa Serikali liendelee kwani lina manufaa makubwa. Umoja huu ni mzuri na unapendeza kwani hapa tunatengeza umoja, mshikamano, upendo na ushirikiano”,amesema Sheikh Makusanya.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amelipongeza na kulishukuru Kanisa hilo kuandaa futari huku akitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa dini kukemea vitendo vya ukatili wa aina zote akieleza kuwa inaleta taswira mbaya mkoa wa Shinyanga kuwa na sifa ya matukio ya ukatili.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani leo Jumanne Aprili 18,2023 katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu upande wa Mahusiano na Dini zingine, Khalid Sadiki Juma akizungumza wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Viongozi wa Dini ya Kiislamu wakichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando
Viongozi wa Dini ya Kiislamu wakichukua Futari wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando (kushoto), Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Hamis (kulia) wakipata futari

heikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiomba dua wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akiomba wakati wa Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoshiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya (kulia) Vitabu vya ‘Jipatie Amani ya Moyo’ 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akizungumza wakati akimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya  zawadi ya Mbuzi na Mchele kwa ajili ya Eid
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akishikana mkono na Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya ishara ya kukabidhi zawadi ya Mbuzi na Mchele kwa ajili ya Eid
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanza Ukanda wa Dhahabu Enoch Marwa Sando akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kushoto) Vitabu vya ‘Jipatie Amani ya Moyo’.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464