NAIBU KAMISHINA TIRA APONGEZA MKAKATI WA BENKI YA CRDB KUCHOCHEA UJUMUISHI WA BIMA KUPITIA CRDB WAKALA

Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Khadija Said (watatu kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya “10 na Kitu” ya Benki ya CRDB inayolenga katika kuadhimisha miaka 10 ya huduma za CRDB Wakala. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Wateja Wago na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul (Wapili Kushoto), Mkuu wa Kitengo cha CRDB Wakala, Ericky Willy (watatu kuli), Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al Barakah, Rashid Rashid (wakwanza kuli), Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya CRDB, Badru Idd, na Meneja wa Ubora na Udhibiti wa Viatarishi TIRA, Zakaria Muyengi.Picha zote na Othman Michuzi.
Dar es Salaam 17 April 2023 – Ikitimiza miaka 10 tokea uanzishwaji wa mfumo wa utoaji huduma wa CRDB Wakala, Benki ya CRDB leo imetangaza kuanzisha huduma za bima kupitia mawakala wake ikiwa ni mkakati wa kusaidia jitihada za Serikali kukuza ujumuishi wa bima nchini.


Mkakati huo umepongezwa na Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), Khadija Said, akisema utakwenda kusaidia kufanikisha lengo la Serikali la kuongeza ujumuishi wa bima kutoka asilimia 15 hivi sasa kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.


“Natambua kuwa Benki ya CRDB ndio kinara kwa idadi ya Mawakala katika sekta ya benki ikiwa na CRDB Wakala zaidi ya 25,000 nchi nzima. Kwa idadi hii nidhahiri kuwa kasi ya ufikishaji na ufikiaji wa huduma za bima itakwenda kuongezeka kwa Kiasi kikubwa,” alisema Naibu Kamishina TIRA huku akiwataka mawakala kufuata miongoz iliyowekwa.


Naibu Kamishina pia aliipongeza Benki ya CRDB kwa mapinduzi makubwa ambayo imeyafanya katika sekta ya fedha nchini katika kipindi cha miaka 10 ya CRDB Wakala. Alisema CRDB Wakala imetoa mchango mkubwa katika kufikisha huduma za fedha kwa wananchi.
Aidha, alipongeza Benki hiyo kwa kuboresha huduma zinazopatikana kupitia CRDB Wakala ambapo sasa hivi wateja wanaweza kupata zaidi ya asilimia 95 ya huduma kupitia mfumo huo ikiwamo huduma ya kufungua akaunti zote za benki ikiwamo akaunti za Al Barakah zinazofuata misingi ya sharia.

“Niwapongeze pia kwa uzinduzi wa kampeni ya ‘10 na Kitu’ ambayo inakwenda kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma zinazotolewa kupitia CRDB Wakala ikiwamo huduma za bima. Niwaombe Mawakala tukashiriki kikamilifu”, aliongezea Naibu Kamishna.
Akielezea kuhusu kampeni ya “10 na Kitu”, Mkurugenzi wa Wateja Wadogo, na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul alisema mbali na kusherehekea maiaka 10 ya CRDB Wakala, kampeni hiyo pia inalenga katika kuhamasisha Mawakala kuongeza kasi ya utoaji huduma kwa kufanya miamala mingi zaidi ili kuchochea ujumuishi wa kifedha.

“Kila mwezi tutakuwa tukitoa zawadi kwa CRDB Wakala ambao watakuwa wamefanya miamala mingi, kufungua akaunti nyingi, na kuuza huduma za bima. Jumla ya zawadi zote katika kampeni hii ni Pikipiki 40, Bajaji 5 na gari aina ya Toyota Alphad kwa mshindi wa jumla,” alibainisha.
Katika kipindi cha maiaka 10, CRDB Wakala imekuwa na mchango mkubwa katika ufikishaji wa huduma za Benki ya CRDB kwa wateja. Bonaventura alisema kuwa takwimu za Benki hiyo zinaonyesha kuwa hivi sasa CRDB Wakala inatoa huduma za kifedha kwa Watanzania zaidi ya milioni 3 kwa mwezi ambapo asilimia 40% ni wateja wa Benki hiyo na asilimia 60 ni wananchi wengine.

Pamoja na mafaniko hayo, taarifa za utendaji za Benki ya CRDB zinaonyesha zaidi ya miamala milioni 100 yenye thamani ya shilingi Trilioni 50 imekua ikifanyika kupitia CRDB Wakala kwa mwaka. Lakini pia, CRDB Wakala imetoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 35,000.




Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd akuzungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya huduma za CRDB Wakala iliyoenda sambamba ya uzinduzi wa kampeni ya “10 na Kitu” ya Benki ya CRDB, iliyofanyika kwenye Ukumbu wa. Golden Memory, Sinza jijini Dar es salaam leo.



Mkuu wa Kitengo cha CRDB Wakala, Erick Willy akuzungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya huduma za CRDB Wakala iliyoenda sambamba ya uzinduzi wa kampeni ya “10 na Kitu” ya Benki ya CRDB, iliyofanyika kwenye Ukumbu wa. Golden Memory, Sinza jijini Dar es salaam leo.



Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al-Barakah, Rashid Rashid akuzungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya huduma za CRDB Wakala iliyoenda sambamba ya uzinduzi wa kampeni ya “10 na Kitu” ya Benki ya CRDB, iliyofanyika kwenye Ukumbu wa. Golden Memory, Sinza jijini Dar es salaam leo.















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464