RAIS WA UTPC,AWATAKA WARATIBU KLABU ZA HABARI KUIMARIKA KIUTENDAJI
Picha ya pamoja ya waratibu wa klabu za habari Tanzania bara na visiwani wakiwa na Mkurugenzi n Rais wa UTPC.
Rais wa Umoja wa Klabu za Habari Tanzania,Deogratius Nsonkolo akizungumza katika mafunzo ya waratibu wa klabu za habari.
Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Habari Tanzania(UTPC),Kenneth Simbaya akizungumza katika mafunzo ya waratibu wa klabu za habari.
Na mwandishi wetu.
Waratibu wa klabu za habari Tanzania wametakiwa kutenda kazi kwa mabadiliko makubwa ili kuweza kuimarisha taasisi ya umoja wa klabu za habari Tanzania( UTPC) ili kuenenda na kasi na kuzingatia maelekezo ya mikakati mpya wa UTPC wa "from Good to Great"
Hayo yamesemwa na Rais wa Umoja wa klabu za habari Tanzania (UTPC),Deogratius Nsokolo akifungua mafunzo ya siku tatu ya waratibu wa klabu za habari Tanzania leo Aprili 18,2023 katika jiji la Dar es salaam.Klabu za habari zipatazo 26 zimeweza kushiriki mafunzo hayo kwa ajili ya kuimarisha utendaji wa klabu hizo.
Deogratius alisema,klabu za habari mkoani ndiyo nguzo za kuimarisha UTPC kwa utendaji ulio na tija kwa mabadiliko yanayohitajika kwa mikakati mpya utakaotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2023 hadi 2025.
Pia Deogratius hakusita kusema hatua za UTPC za katika kuondoa waratibu watakao kwamisha safari ya UTPC katika usimamizi wa fedha zitakazopelekwa katika klabu.
"Tunatakiwa kuanza safari pamoja na kutokwamishana na vema fursa hii ya mafunzo iweze kutumika kuitoa taasisi yetu katika hatua nzuri ya mabadiliko yenye tija zaidi"Anasema Deogratius.
"Waratibu ni wakurugenzi wa Klabu za habari na hamko kwa bahati mbaya ni vema kutumia nafasi yako vizuri ilo kuleta mabadiliko kwa kuwa na ubinifu,uadilifu,nidhamu na kutunza siri za ofisi"Anasema Deogratius.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Umoja wa Habari Tanzania(UTPC),Kenneth Simbaya anasema,tunahitaji kuwa na ushindi kwa kiwango cha juu katika kazi zetu na nyie waratibu ni nguzo ya UTPC na wajibu kuzingatia mafunzo haya kwa umakini.
"Wote tunanufaika katika mafunzo kwa maisha binafsi na taasisi pia,ni vema tuwe katika darasa kwa umakini na kuweza kunufaika"Anasema Kenneth Simbaya
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464