VIONGOZI WA DINI WATAHADHARISHA SERIKALI JUU YA MIKATABA YA USHOGA
Na mwandishi wetu.
Baadhi ya viongozi wa dini nchini wameendelea kukemea vitendo vibaya ya ushoga na ndoa ya jinsia moja katika jamii ya watanzania,kauli hizo zimetolewa katika kuaazimisha sikuuu ya pasaka kwa waumini wa kikristo nchi Tanzania.
Hayo yameelezwa katika ibada ya pasaka,jumapili,Aprili9,2023 katika kanisa la IEAGT( International Evangelical Assemblies of God Tanzania)la manispaa ya Shinyanga na Mchunga Dk.Timothy Mwantake akisema, hakubaliani na ushoga na ndoa ya jinsia moja kwani ni ushetani mbele za Mungu.
Mwantake anasema,hatakubali na ataendelea kushirikiana na viongozi wengine wa dini kwa ujasiri mkubwa katika majukwaa mbalimbali ya dini na hata ya siasa kupinga hali hiyo kwani anamtetea Mungu pia na kizazi cha watanzania.
"Ushoga na ndoa ya jinsia moja ni upumbavu na ujinga kwa watu wote wanaoukubali kwani ni laana na hila ya ibilisi kwa Taifa letu na vizazi vyetu"Anasema Dk. Mwantake.
Kwa upande mwingine,DK.Mwantake anasema ikiwa kuna wafadhili wanao kuja kwa Taifa letu na kutoa k fedha kwa masharti na mikataba ya ushoga na ndoa ya jinsia moja ni vema serikali ikatae hayo kwa masilahi ya vizazi vya watanzania na hata utukufu wa Mungu juu ya nchi hii.
" Hakuna namna nyingine kusema wazi mapema kwa sasa kuhusu serikali ikiwa italazimishwa na watu wa mataifa ya magharibi kupokea fedha zenye uchafu mbele za Mungu na watu wake,Tutasimama kwa ujasiri kukemea hilo na wala hatutaogopa kuisemea hiyo dhambi wazi wazi na hata kuandamana na waumini wetu"
Nao baadhi ya waumini wa kanisa hilo,Silvesta Kahema,walisema ni wakati wa wazazi kuweka nguvu kwa kumtegemea Mungu na kuiombea serikali ili isishawishiwe na watu wenye hila la ibilisi kutoka mataifa ya nje kwa misaada yenye masharti mabaya.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464