WATANZANIA WATAKIWA KUPENDA IBADA NA MAOMBI ILI KUIMARISHA NGUVU ZA KIROHO NA KUIMARISHA UTAKATIFU

Mchungaji na Mwinjilisti Edward Mtinda wa kanisa la Tanzania Assemblies of God TAG Mwanza akihubiri neno la Mungu katika kanisa Philadelphia Miracle Temple lililopo mjini Shinyanga


Suzy Luhende,Shinyanga Blog

Watanzania wametakiwa kupenda ibada na maombi kwa sababu ibada zinaongeza nguvu za kiroho na zitawasogeza karibu na Mungu, na Ibada huimarisha utakatifu ndani ya maisha ya mwanadamu.

Hayo ameyasema mchungaji Edward Mtinda wa kanisa la Tanzania Assemblies of God TAG Mwanza alipokuwa akiendesha semina ya siku tatu ya neno la Mungu katika kanisa la Philadelphia Miracle Temple lililopo mjini Shinyanga, ambapo amewataka watanzania kupenda ibada na maombi ili kuwa na nguvu za kiroho na kuweza kukemea maovu.

Mtinda ambaye ni mwinjilisti wa kimataifa akifundisha somo la Umuhimu wa ibada katika siku ya pili ya semina amesema waumini wengi wamekuwa hawahudhurii ibada katika makanisa hali ambayo imekuwa ikidhoofisha nguvu ya koroho,lakini Mungu ni Mungu wa ibada husema na watu ndani yaibada anaonya anaponya na anabariki ndani ya ibada.

"Matendo ya mitume 13:2-3 inasema 
basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia, ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao"amesema Mchungaji Mtinda.

Amesema usipokuwa mtu wa kuhudhulia ilbada kuna viwango hautafikia na bila ibada hautafika mbinguni, kwani ibada huimarisha utakatifu ndani ya moyo wako pia pasipo ibada utakuwa humtendei haki Mungu wako aliyekuumba au aliyekuokoa.

"Ibada ndiyo haki pekee ya ukombozi wako, kitu chochote cha ntu asiyefa ya ibaada kitakosa ulinzi wa Mungu na Yesu alituokoa ili tuwe vyombo vya ibada, hivyo tunatakiwa tuwe watu wa kupenda ibada ili Mungu aweze kutubariki na kuweka ulinzi katika mali zetu,"amesema mchungaji Mtinda.

Aidha mchungaji Mtinda amesema kuna aina mbili za ibada ibada za kawaida, mathayo 15:7-9 ibada za haki Yohana 4:23-24 Mungu anaagiza kuheshimu sana ibada, pia anaagiza uongeze upendo kwenye ibada na usikose kamwe ibada kwani majibu pekee yanatoka kwa Mungu.

"Usipomfanyia Mungu ibada anakuhesabia kama umetenda dhambi tano, hivyo unakuwa unamfanyia Mungu ujeuri na una kiburi cha uzima, unamvunjia Mungu heshima, unadhambi ya dharau,una majivuno unajivunia uhai ulionao ambao ni mali ya Mungu, hivyo unatakiwa kubadilika na kutengeneza muda wa kumwabudu Mungu yaani kwenda ibadani,"amesema Mtinda.

Pia amesema Mungu anahitaji watu wanaomwabudu katika Roho na kweli "njoo ibadani ukutane na Mungu wako ili aweze kutatua matatizo mbalimbali uliyonayo, ukiwa mwaminifu katika ibada na ukamta guliza yeye atakutendea na baraka zake utaziona"amesema Mtinda

Kwa upande wake mchungaji kiongozi wa kanisa la Philadelphia Miracle Temple Baraka Laizer lilopo kata ya Ndembezi mjini Shinyanga amewataka waumini wa kanisa hilo waheshimu ibada na wapende kuhudhuria ibada ili waweze kubarikiwa.
Mchungaji Edward Mtinda akiendelea kuhubiri katika kanisa la Philadelfia Miracle Temple
Kazi ya mahubiri ikiendelea 
Mchungaji Edward Mtinda akiombea waumini wa kanisa la Philadelfia baada ya kumaliza kuhubiri
Mchungaji Baraka Laizer akiombea waumini wa kanisa hilo
Mchungaji Edward Mtinda akiombea waumini wa kanisa la Philadelfia baada ya kumaliza kuhubiri
Mchungaji Edward Mtinda akiombea waumini wa kanisa la Philadelfia baada ya kumaliza kuhubiri
Mchungaji Baraka Laizer akiwataka waumini wa kanisa hilo kuheshimu ibada ili Mungu aweze kuwatendea yaliyo mema waumini wa kanisa hilo
Mchungaji wa Baraka Laizer akiwa kwenye picha ya pamoja na mchungaji Edward Mtinda
Ma mchungaji Evarine Msangi akiwa ndani ya kanisa baada ya kumaliza kuongoza sifa na kuabudu 
Wanakwaya wa kanisa la Philadelfia wakiwa wanaimba kwenye ibada iliyofanyika kanisani ha
Kwaya ikiendelea kumsifu Mungu
Mchungaji Baraka na baadhi ya viongozi wa sifa na kuabudu wakimsifu Mungu kwa matendo yake makuu
Wakimsifu Mungu
Maombezi yakiendelea baada ya neno la Mungu
Waumini wa kanisa hilo wakisikiliza neno la Mungu
Emmanuel Hezron na Ifraimu Annord wakisikiliza neno la Mungu
Steven Hezron akimwimbia Mungu
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464