Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo akiwa wilayani Kishapu kuangalia utekelezaji wa miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
Na Marco Maduhu, KISHAPU.
WAZIRI wanchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk. Seleman Jafo, ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi (EBARR) wilayani Kishapu.
Jafo amebainisha hayo leo Mei 6,2023 wakati alipofanya ziara wilayani Kishapu, kutembelea kuona utekelezaji wa miradi hiyo ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
Amesema katika ziara yake wilayani Kishapu ya kutembelea miradi hiyo ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, ameridhika nayo baada ya kuona imetekelezwa vizuri, huku akiagiza kwa ile ambayo bado haijakamilika ikamilike haraka kabla ya mwaka wa fedha mwezi Julai iwe tayari na kuanza kutumika.
“Nimeridhika na ziara yangu hapa Kishapu nimeona miradi iko vizuri, na Rais Samia anapoona miradi ambayo anatoa fedha inatekelezwa vizuri anafarijika sana,”anasema Waziri Jafo.
“Naomba wananchi muitumie vyema miradi hii kwa tija, pamoja na kutunza mazingira kwa kupanda miti,”ameongeza.
Aidha, Miradi ambayo Waziri Jafo ameitembea ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi pamoja na mingine kuweka jiwe la msingi na kuzindua ni Mradi wa unenepeshaji Mifugo katika Kijiji cha Muguda, na kuweka jiwe la msingi katika jengo la kusaga mahidi na kukamua Alzeti, Bwawa la Maji Kijiji cha Kiloleli na Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi vikiwamo viatu.
Miradi mingine ambayo inatekelezwa ni ujenzi wa Majosho, Majiko Banifu yatakayosaidia kupunguza matumizi ya kuni, ufugaji wa nyuki, na kilimo zao la Mkonge,
Anesema Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kutekelezwa miradi hiyo ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, ili wananchi wawe na shughuli mbadala za kufanya ambazo zitawaingizia kipato na kuacha kuharibu mazingira kwa kukata miti hovyo ikiwamo kufanya biashara za kuchoma mikaa.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo, ameziagiza halmashauri zote hapa nchini kutekeleza agizo la upandaji miti Milioni 1.5 kwa kila mwaka, pamoja na kuihamasisha kampeni ya soma na mti ambayo kila mwanafunzi anapaswa kupanda mti.
Naye Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, amesema Serikali ilipeleka kiasi cha fedha Sh.bilioni 1.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi. ambayo inatekelezwa katika Kata mbili ya Lagana na Kiloleli, na imekuwa na tija kwa wananchi katika suala zima la utunzaji wa Mazingira.
Nao baadhi ya wananchi ambao ni wanufaika wa miradi hiyo, wameishukuru Serikali kwamba licha ya kutunza mazingira, pia imekuwa ikiwasaidia kuwaingizia kipato na kuendesha maisha yao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo akizungumza wilayani Kishapu akiwa kwenye ukaguzi wa miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na baadhi kuweka jiwe la msingi na mingine kuizindua.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo akizungumza wilayani Kishapu akiwa kwenye ukaguzi wa miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na baadhi kuweka jiwe la msingi na mingine kuizindua.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye ziara hiyo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Anderson Mandia akizungumza kwenye ziara hiyo ya Waziri Jafo.
Mratibu wa mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi (EBARR)wilayani Kishapu Godwin Everygist akitoa taarifa juu ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo (kushoto) akiweka jiwe la msingi katika Jengo la Mashine ya Alizeti na kusaga Mahindi katika kijiji cha Muguda, mradi ambao utatumika pia kunenepesha mifugo kupitia mapumba.
Muonekano wa jiwe la msingi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo akipanda mti mara baada ya kumaliza kuweka jiwe la msingi jengo la mashine ya kukamua Alizetu na kusaga Mahindi, katika mradi wa kunenepesha mifugo kupitia pumba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo (kushoto) akizindua kiwanda kidogo cha kutengeneza bidhaa za ngozi (kulia) ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.
Muonekano wa jiwe la msingi la uzindizi wa kiwanda hicho cha kutengeneza bidhaa za ngozi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo (kushoto) akiangalia bidhaa mbalimbali ambazo zimetengenezwa kwa ngozi.
Muonekano wa viatu ambavyo vimetengenezwa kwa kutumia ngozi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo akiangalia kiatu ambacho kimetengenezwa kwa ngozi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo akiwa amevaa viatu ambavyo amevinunua vilivyotengenezwa kwa ngozi na kutoa wito kwa wananchi wa Kishapu na Taasisi za Serikali kukiunga mkono kikundi hicho na kununua viatu.
Muonekano wa bwawa la maji ambalo limetekelezwa katika kijiji cha Kiloleli katika mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo (kushoto) awali akiwasili wilayani Kishapu akisalimiana na viongozi mbalimbali (kulia) ni Mkurugenzi wa Halamshauri ya Kishapu Emmanuel Jonhson, akifuatiwa na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Anderson Mandia.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Seleman Jafo (kushoto)akiendelea kusalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili wilayani Kishapu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464