BENARD MEMBE AFARIKI DUNIA
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Mhe.Bernard Kamilius Membe, amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Kairuki mkoani Dar es Salaam.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa alipata changamoto ya kifua na kupelekwa alfajiri ya leo Hospitalini hapo na baadaye kufariki.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha hospitali ya Kairuki, Arafa Juba amethibitishia Mwananchi taarifa za kutokea kwa kifo hicho akieleza kuwa kimetokea saa mbili asubuhi.
“Ni kweli Membe aliletwa asubuhi hapa akapatiwa matibabu na wataalam kama ilivyo kawaida mgonjwa anapokuja hospitali, lakini Mungu alimpenda zaidi akafariki saa mbili asubuhi,” amesema Arafa.
Chanzo: ITV Tanzania
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464