DC MKUDE ATOA MAAGIZO MAZITO KWA WANUNUZI WA PAMBA WILAYANI KISHAPU

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude , amewataka Wanunuzi wa Zao la Pamba wilayani humo kuzingatia Taratibu na sheria zilizowekwa za ununuzi wa Pamba katika Wilaya ya Kishapu.

Mkude ameyabainisha hayo leo Mei 18, 2023 wakati alipofanya kikao kazi na Wenyeviti na Makatibu wa Amcos pamoja na wawakilishi wa Makampuni yanayonunua Pamba.

Amesema katika Wilaya ya Kishapu Kuna utaratibu waliojiwekea kwenye ununuzi wa zao la Pamba ikiwemo kibali Maalum au leseni ya ununuzi wa Pamba.

“Natoa wito kwa Makampuni yote ya ununuzi wa Pamba kuwa na kibali Maalum au leseni ya ununuzi wa Pamba hivi ni vitu vya kuzingatia kuvunja Taratibu ni kinyume cha Sheria Tuwe na na nidhamu wakati wote tunapofanya Shughuli zetu za ununuzi wa Pamba tuzingatie Sheria ili kuepuka malalamiko kwa wananchi, tuzingatie muongozo na Mkataba uliotolewa na Mkurugenzi." amesema

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Ndugu. Mang'era Mang'era, amesema ni muhimu kwa Makampuni kulipa Ushuru wa Halmashauri kwa wakati kama Sheria inavyosema

" Wito wangu kwa Makampuni yote ni kulipa Ushuru wa Halmashauri kwa wakati ndani ya masaa 48 kama Sheria inavyotaka hii itaweka mazingira rafiki kwa Halmashauri na mnunuzi pia kwa Mwaka huu ni vyema sasa tukazingatia Sheria na Taratibu za ununuzi tuliojiwekea katika msimu huu." Alisema Mang'era

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirecu Ndugu Josephat Limbe amesema kuwa Malipo ya Ushuru kwa Makampuni unatakiwa kufanyika ndani ya Masaa 48, hivyo ameyataka Makampuni kuzingatia Taratibu na miongozo ili kuondoa usumbufu ambao unajitokeza mara kwa mara.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464