Mkuu wa wilaya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye kikao hicho.
Na Frank Mshana, KISHAPU
Kamati za ufuatiliaji wa matumizi ya raslimali za Umma, public expenditure tracking system (PETS) wilayani kishapu zimebaini kuwa asilimia kubwa ya jumuiya za watumia maji mijini na vijijini haziwasomei wananchi mapato na matumizi huku serikali ikiombwa kuzisaidia na kuwezesha kamati hizo kufuatilia miradi mingi zaidi kwa manufaa ya jamii.
hali hiyo ni changamoto mojawapo kati ya changamoto kadhaa zilizobainishwa katika kikao cha kuwasilisha na kujadili taarifa ya kamati za ufuatiliaji matumizi ya raslimali za umma katika utekelezaji wa miradi ya maji wilaya ya kishapu.
akiwasilisha taarifa za kamati za PETS kwenye baadhi ya vijiji vya wilaya ya kishapu mwezeshaji wa shirika kisilo lakiserikali linalojihusisha kutoa misaada yakibinadamu ikiwepo utunzaji wa mazingira na upatikanaji wa majisafi na salama katika maeneo yenye ukame bwana Stephen Rusindi amesema katika ufuatiliaji wa miradi ya maji kamati zimebaini mapungufu mbalimbali ikiwemo maji kukatika kwa baadhi ya vituo vya kuchotea maji.
Baadhi ya venyeviti wa vijiji vyenye miradi ya maji iliyopitiwa na kufuatiliwa na kamati za PETS wamesema ufuatiliaji huo umewafungua macho wananchi na kuomba ufuatiliaji huo uendelee kwa miradi yote inayojengwa kwa fedha za serikali pamoja na wafadhili ili kupata thamani halisi ya miradi hiyo.
Oscar Rutenge ni kiongozi wa miradi ya TCRS Kishapu amesema shirika la TCRS lina miradi mitano inayoendeshwa katika wilaya ya kishapu ambayo ni, mradi wa kujengea jamii uwezo jumuishi unaofanyika katika kata ya mwakipoya,shagihilu,ndoleleji na masanga na kujumuisha vijiji kumi na tano, usalalama wa chakula na kukuza uchumi unaotekelezwa katika kata ya Mondo na Sekebugolo mradi ambao unaotekelezwa kwenye vijiji 10 vya kata hizo.
Miradi mingine ni kilimo cha usatahimilivu na kukuza uchumi unaotekelezwa katika kata ya ndoleleji na sekebugolo kwenye vijiji 10, kuimarisha ulinzi na haki kwa wasichana, wanawake vijana pamoja na wenye ulemavu unaotekelezwa kwenye kata 10 za wilaya ya kishapu na kujumuisha vijiji 44, mradi wa kuboresha upatikanaji wa maji kupitia uwazi katika kata tano wilayani kishapu ambapo unajumuisha vijiji 10 ukitekelezwa na kamati za pets zilizojengewa uwezo na shirika la TCRS kwa ufadhili wa shirika la Foundation for Civil Society (FCS).
msimamizi wa miradi ya TCRS Bi. Kellen machibya ameishukuru serikali kutoa ushirikiano katika miradi yakijamii inayotekelezwa na shirika hilo huku akiomba ushirikiano huo uendelee kwa malengo ya kuleta maendeleo yenye tija kwa wananchi wanaoishi katika maeneo yenye changamoto mbalimbali.
Baadhi ya madiwani wa kata zenye miradi ya maji inayoendelea na iliyokamilika wametoa rai kwa madiwani wengine na wenyeviti wa kata na vijiji kuhakikisha kuwa swala la maji wanalichukulia uzito stahiki na kuhakikisha kuwa wanachi wanapata huduma bora kulinagana na mahitaji yao huku makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kishapu ambaye pia ni diwani wa kata ya ukenyenge mheshimiwa Anderson mandia akiitaka mamlaka ya maji na usafi wa mazingira kutoa taarifa sahihi mapema kabla ya kukata maji kwa ajili ya kufanya marekebisho au matengenezo ya mabomba ya maji ili kupunguza usumbufu na malalamiko ya wananchi kwa kukosa maji ghafla.
Meneja wa Ruwasa wilayani kishapu Mhandisi Dickson Kamazima amesema changamoto baadhi zinazokwamisha maendeleo ya miradi ya maji na kudumaza utoaji wa huduma bora ni baadhi ya taasisi za Serikali kutolipa ankara (bili) za maji ambapo amedai kuwa zoezi linalofuata sasa ni kukata maji kwa yeyote anayedaiwa kwakuwa uendeshaji wa huduma za maji unahitaji fedha nyingio.
Aidha afisa maendeleo ya kamii mkoa wa shinyanga bwana Tedson Ngwale amekiri kuwa shirika la TCRS limefanya kazi kubwa kwa wilaya ya kushapu kuchagiza maendeleo ya jamii kupitia miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya maji huku akidai kuwa kazi hizo zimeisaidia sana Serikali kuhakikisha kuwa dhana ya kumtua mama ndoo kichwani inatekelezeka huku akidai kuwa bado kuna kazi ya kufanya kuwaelimisha wananchi juu ya kulinda na kutunza vyanzo vya maji na kushauri kuwa taarifa za pets ziwe ni sehemu ya maboresho ya utekelezaji wa miradi ya maji.
Mkuu wa wilaya ya kishapu Joseph Mkude amewahakikishia wadau wa maendeleo kama vile TCRS na taasisi zingine na kuwahakikisha kuwa uwazi na uwajibikaji kwenye sekta ya maji inapewa msukumo mkubwa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma ya maji ya kutosha.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye kikao hicho.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu Mhandis Dickson Kamanzima akizungumza kwenye kikao hicho.
Meneja Miradi TCRS Kellen Machibya akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464