SERIKALI YATOA MABILIONI YA FEDHA KUKAMILISHA UJENZI UWANJA WA NDEGE IBADAKULI MANISPAA YA SHINYANGA

SERIKALI imetoa kiasi cha fedha zaidi Sh billioni 49.1 kwaajili ya kukamilisha ukarabati uwanja wa ndege uliopo Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga utakao chukua miezi 18 kukamilika kwake.
Taarifa hiyo imetolewa leo Mei 30, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme katika mkutano wa wadau wa usafirishaji wa anga na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Shinyanga.
Samizi amesema watu wa Shinyanga wamekuwa na shauku kubwa ya kupata uwanja wa ndenge kwani walikuwa wakilazimika kusafiri kwenda mkoani Mwanza kupanda ndege umbali wa kilomita 164.

“Wadau wa Mkoa wa Shinyanga Sasa wafahamu fursa zilizopo ndege zikianza kufanya kazi kwani uchumi wa mkoa huu utakuwa kwani Ndege zitakazo kuwepo zitaweza kuchukua abiria 150 hadi 250 kwa wakati mmoja”alisema Samizi.
Meneja mradi viwanja vya ndege,Tanroads kutoka makao makuu mhandisi Neema Joseph amesema Uwanja huo utafanywa maboresho makubwa utakuwepo upanuzi wa uwanja kilomita mbili upanda mita 800, jengo la kusubiria abiria awali halikuwepo njia zitakazojengwa kiwango cha Lami.
“Ujenzi huo utasimamiwa na wahandisi kutoka kampuni ya SMEC ya nchini Australia na kujengwa na kampuni ya CHICO kutoka nchini China”amesema Mhandisi Joseph.

PICHA NA KADAMA MALUNDE

SOMA HAPA ZAIDI CHANZO HABARI LEO.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464