DC MKUDE AFANYA ZIARA KUKAGUA UJENZI WA MATUNDU YA VYOO SHULE ZA MSINGI KISHAPU


Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe.Joseph Mkude, amefanya ziara katika Shule za Msingi Mwalata na Ng'wandu wilayani Kishapu, ya kukagua ujenzi wa Matundu ya vyoo 36 ambayo yanayojengwa kwenye Shule hizo,

Mkude akizungumza katika ziara hiyo jana Mei 17,2023 amesema ametembelea Shule hizo, ili kuona namna shughuli za ujenzi zinavyoendelea pamoja na kuona hatua ambayo wamefikia ya ujenzi wa Matundu ya vyoo,

Aidha, Mkude amesema ameridhishwa na kasi ya Ujenzi pamoja na Ubora kwa Shule zote zenye miradi hiyo

"Katika ujenzi wa Matundu haya nimeridhishwa kazi ni nzuri sana na kasi inakwenda Vizuri Miradi hii anayotoa Mhe. Rais ina tija kubwa kwa Watoto wetu lengo kubwa watoto ni kunawa ili kuepuka na Magonjwa kama Vile Covid-19, Kipindupindu na itasaidia kwa kizazi hiki kuchukia kujisaidia polini na badae kuwa wazazi bora kwa kujenga nyumba zenye vyoo Bora kwa kuwa nyumba ni Choo."

Katika hatua nyingine Mkude amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Ndugu Emmanuel Johnson kwa kusimamia vyema katika suala la ushirikishwaji wa Wananchi katika Miradi inayoendelea kwenye Halmashauri kwa Sababu kila anapopita Wananchi wanaitambua Miradi na wanakuwepo eneo la Mradi kila wakati pamoja na kuundwa kamati za Ujenzi ambazo zinawananchi wa Maeneo husika.

Aidha, amewataka wananchi ambao wapo kwenye kamati za Ujenzi kuwa wasimamizi Bora wa Miradi,ili Miradi iweze kukamilika kwa wakati na Ubora unaohitajika ili iweze kuwanufaisha watoto kwa muda mrefu.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464