Dk.Martine Masalu (kushoto) akimkabidhi mmoja wa wazazi Kadi za Bima ya Afya CHF kwa niaba ya Taasisi ya Nancy Foundation.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
TAASISI ya Nancy Foundation imetekeleza adhima yake ya kuwakatia Bima ya Afya (CHF) iliyoboreshwa, watoto ambao waliwaokoa waliokuwa wakiishi mitaani katika Manispaa ya Shinyanga, ili kuwarahisishia upataji wa huduma za matibabu bure na kuokoa afya zao.
Zoezi hilo la kukabidhi kadi hizo za CHF limefanyika leo Mei 12, 2023 katika viwanja vya mazingira center Manispaa ya Shinyanga.
Dk. Martine Masalu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, akizungumza kwa niaba ya Taasisi ya Nancy Foundation, amesema suala la Afya ni muhimu sana, ndiyo maana Taasisi hiyo imeamua kuwakatia Bima ya Afya (CHF) ambayo itakuwa msaada mkubwa katika kuokoa Afya zao.
“Taasisi ya Nancy Foundation imempatia Shilingi 120,000 Mwandikishaji wa CHF Manispaa ya Shinyanga, ili atukatie Kadi za Bima ya Afya, na tunazikabidhi Kadi hizi leo leo kwa wazazi wa watoto hawa ambao walikuwa wakiishi mitaani, ili kuwarahisishia upataji wa matibabu bure,”amesema Dk.Masalu.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Nancy Foundation Ezra Manjerenga, amesema Kadi hizo za CHF zitakuwa pia msaada kwa familia nzima ya watoto hao kupata matibabu bure.
Amesema licha ya watoto hao kuwakatia Bima hiyo ya Afya CHF watawalipia pia huduma ya chakula shuleni, pamoja na masomo ya ziada (tuition) ili wasome katika mazingira rafiki.
Nao baadhi ya wazazi wa watoto hao akiwamo Farida Kasigwa, wameishukuru Taasisi hiyo ya Nancy Foundation kwa kuwasaidia kuwatoa watoto wao kuishi mitaani, kwamba wengine walikuwa tayari wameshawapoteza watoto na hawakujua mahali walipo, lakini sasa wanaishi nao, na kushukuru kukatiwa Kadi ya Bima ya CHF ambayo itawasaidia kupata huduma ya matibabu bure.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nancy Foundation Ezra Manjerenga akizungumza kwenye zoezi la kukabidhi Kadi za Bima ya Afya CHF kwa wazazi wa watoto ambao walikuwa wakiishi mitaani katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwandikishaji wa CHF Manispaa ya Shinyanga Mary Budigisila akizungumza kwenye zoezi hilo la kukabidhi Kadi za CHF kwa wazazi ambao watoto wao walikuwa wakiishi mitaani.
Mmoja wa wazazi akishukuru kukatiwa Bima hizo za Afya CHF watoto wao ambao pia zitawasaidia na wao kupata huduma za matibabu bure.
Dk.Martine Masalu (kushoto) akimkabidhi fedha Sh.120,000 mwandikishaji wa Bima ya afya CHF Manispaa ya Shinyanga Mary Budigisila kwa niaba ya Taasisi ya Nancy Foundation kwa ajili ya kukata Kadi za Bima za Afya na kuzikabidhi kwa watoto wazazi ambao watoto wao wailikuwa wakiishi mitaani kabla ya kuokolewa na Taasisi ya Nancy Foundation.
Dk.Martine Masalu (kushoto)akikabidhiwa Kadi za Bima ya Afya CHF na Mwandikishaji wa Bima ya Afya CHF Manispaa ya Shinyanga Mary Budigisila kwa niaba ya Taasisi ya Nancy Foundation kwa ajili ya kuzikabidhi kwa wazazi ambao watoto wao wailikuwa wakiishi mitaani kabla ya kuokolewa na Taasisi ya Nancy Foundation.
Dk.Martine Masalu (kushoto) akimkabidhi mmoja wa wazazi Kadi za Bima ya Afya CHF kwa niaba ya Taasisi ya Nancy Foundation.
Zoezi la kukabidhi kadi za Bima ya Afya CHF likiendelea.
Watoto ambao walikuwa wakiishi katika mitaani Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa Bima ya Afya CHF, Kadi ambazo wamepewa wazazi wao kwa niaba yao ili kuwasaidia kupata huduma ya matibabu bure.
Baadhi ya wazazi ambao watoto wao walikuwa wakiishi mitaani wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa Kadi za Bima ya Afya CHF kwa niaba ya watoto wao.
Baadhi ya wazazi ambao watoto wao walikuwa wakiishi mitaani wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa Kadi za Bima ya Afya CHF kwa niaba ya watoto wao.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464