CHADEMA- YAMSIMAMISHA MWENYEKITI WA MKOA WA SHINYANGA

Na. Mwandishi wetu.

Kamati tendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kanda ya serengeti imemsimamisha uongozi Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga  Mhe.Emmanuel Ntobi kutokana na makosa ya nidhamu.

Tukio hilo la kumsimamisha mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga wa chama cha demokrasia na maendeleo,(chadema)Mhe.Emmanuel Ntobi limeelezwa na katibu wa kamati ya uenezi,Golden Charles Marcus leo Mei 2,2023 wakati akiongea na Shinyanga Press Club blog.

Golden anasema ni kweli barua hiyo inayosamba katika mitandao ya jamii ni sahihi kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema) inayomhusu Mhe. Emmanuel Ntobi,ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Shinyanga.

"Taratibu za chama zinampa nafasi mhusika kukata rufaa ya  ndani ya siku the lathini,Ntobi ni mwanasiasa mkongwe anajua hatua zote za kuzingatia kuhusu rufaa yake na ana tambua  yote juu ya barua hiyo kwa kuwa vikao halali alishirikishwa hadi hatua ya mwisho ya barua hiyo kutolewa na uongozi wa chadema "Anasema Golden

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464