CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA- KOLANDOTO NA WADAU WAMEENDESHA MDAHALO JUU YA KUPOROMOKA KWA MAADILI NCHINI.

 

CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA- KOLANDOTO  NA WADAU WAMEENDESHA MDAHALO  JUU YA  KUPOROMOKA KWA MAADILI NCHINI.

Picha ya pamoja ya viongozi wa chuo na wadau kutoka manispaa ya Shinyanga

Afisa Habari na Mahusiano wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto-Josephine Charles,akiwaongoza mdahalo wa mmomonyoko wa maadili chini
Msimamizi wa dawati la jinsia chuo cha sayansi za afya Kolandoto,Digna Michael akizungumzia kuhusu wanavyo simamia maadili katika chuo hicho.
 Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma bw. Eliakimu Ole-Saitabau cha sayansi ya afya kolandoto akizungumza katika mdahalo wa mmomonyoko wa maadili.

 
Kaimu Mkuu wa Chuo cha sayansi za Afya -Kolandoto ,Michael Hernico,akifungua mdahalo uliohusu hali ya mmomonyoko wa maadili chini


Mchungaji Joel Mginya -Kanisa la AICT -tawi la Kolandoto chuoni akiwasilasha mada namba 01 ya namna  chimbuko la mmonyoko wa maadili kwa mujibu wa neno la Mungu.
Mwenyekiti wa Makundi Maluum Taifa-SIMAUJATA,Bi.Sophia Kang'ombe akiwasilisha mada namba 02  ya namna  saikolojia ya tabia inavyo athiri mmonyoko wa maadili.
Afisa ustawi Mkoa wa Shinyanga ,Lydia Kwesigabo akiwasilisha mada ya  namba 03 ya namna ya malezi na makuzi yanavyo athiri mmonyoko wa maadili

Afisa Maendeleo Mkoa wa Shinyanga.Tedson Ngwale akiwasilisha mada ya  namba 04 namna maendeleo yanavyo athiri mmonyoko wa maadili.


Mkuu wa dawati la jinsia -jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga .SSP Monica Sahere akiwasilisha mada namba 05 ya ukubwa  wa mmomonyoko wa maadili na madhara yake.



Wanafunzi wa chuo cha sayansi za afya -kolandoto wakitoa maoni yako katika mjadala wa mmomonyoko wa maadili nchini.



Wanafunzi wa chuo cha sayansi za afya -kolandoto wakisikiliza

Mwandishi wetu.

Chuo Cha Sayansi ya Afya Kolandoto kimeendesha mdahalo uliohusu  hali ya mmomonyoko wa maadili nchini  kwa kushirikiana na wadau kutoka mkoa wa Shinyanga ili kuweza kujadili hatua mbalimbali zinaoweza kuchukuliwa na jamii na serikali ili kuepusha athari mbalimbali zinazokabili nchi yetu.

Mdahalo huo wa umefanyika leo Mei 13,2023 kwa katika chuo cha sayansi za afya-kolandato kilichopo mansipaa ya Shinyanga  kwa kushirikisha wadau mbambali kutoka mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kujadili hali ya mmomonyoko wa maadili nchini..

Wadau waliweza kushiriki ni jeshi la polisi,maafisa ustawi na maendeleo ngazi ya mkoa,watendaji ngazi ya kata,viongozi wa dini,wananchi wa manispaa ya Shinyanga na waandishi wa habari.

Kaimu Mkuu wa Chuo Sayansi za Afya kolandoto,Michael Henerco anasema kuwa mdahalo huo ni agizo la serikali ya Tanzania katika kujadili hali ya mmomonyoko wa maadili nchi na unatekelezwa katika vyuo vyote na leo chuo cha kolandoto kimechukua hatua.

"Tulifurahishwa na agizo la serikali kwa ajili ya kujadili hali ya mmonyoko wa maadili kwa kuwa kila mmoja hapa anaguswa na athari hizi na tumealika wataalam wabobezi wa masuala haya  ili  ya kuweza kujadiana na kupata  maoni kwa washiriki kutoka makundi mbalimbali"anasema Henerco

"Tunaomba washiriki wote kuweza kutoa maoni ili tuweze kujifunza na tuondoke hapa tukiwa mabalozi kwa kusimamia jamii  yetu kuhusu hali ya maadili na si wakati  kunyamaza kwa hali maadili ilivyo kwa sasa  kwa kuwa kila moja wetu hili lina mhusu"Anasema Henerco.

Mjadala huo uliwapa nafasi wataalam kutoka sekta mbalimbalk kuwasilisha mada zinazohusu hali ya mmonyoko  wa maadili kwa makundi ya uwakilishi wao.

Mchungaji Joel Mginywa kanisa la AICT -tawi la kolando chuoni ,akiwasilisha mada ya Chimbuko la kuporomoka wa maadili kwa mujibu wa neno la Mungu,anasema kuwa watu hawana hofu ya Mungu na wanawake wana changamoto  wanapotafuta nafasi za kitaaluma  au kazi ,wanaobwa rushwa ya ngono.

"Ni wakati wa kuungama na kutubu kwa kumrudia Mungu ili atusadie katika hali hii ya kasi ya mmonyoko wa maadili na jamii kumfuata Yesu kristo"anasema Joel.

Sophia Kang'ombe ,Mwenyeki wa makundi maalum Taifa,anasema akiwasilisha mada ya saikolojia inavyo athiri tabia,alibainisha kuwa urithi wa vinasaba vya wazazi,akili,mazingira na utu wa mtu unaweza kuleta kuporomoka wa maadili kwa kuathiri maamuzi yake ya mwisho ya kutenda jambo jema au zuri kwa mwingine.

"Tabia yoyote ile mbaya inaweza kuondolewa kwa mtu kwani mwanadamu ana uwezo wa kubadilika,ni vema kuweza kuendele kuwaelimsha watu"anasema Sophia.

Naye Afisa ustawi Mkoa wa Shinyanga,Lydia Kwesgabo akiwasilisha mada ya malezi na makuzi yanayovyochangia kuporomoka wa maadili,anasema uwajibikaji hafifu,jamii kutowajibika kama zamani kusaida watoto,umaskini wa kipato,ukosefu wa hofu ya Mungu na migogoro ya ndoa ni chanzo cha mmomonyoko wa maadili katika jamii.

"Wana ndoa waepuke migogoro na watenge muda wa ziada wa kulea watoto na wakubaliane idadi ya watoto wanaoweza kuwalea kadri ya kipato chao na hata kuepuka kuiga maisha ya mitandao ya jamii ili tusiharibu watoto"Anasema Lydia.

Kwa upande wake,Afisa Maendeleo  ya Jamii  mkoa wa Shinyanga,Tedson Ngwale,akiwasilisha mada ya  maendeleo yanavyoweza kuchangia kuporomoka wa maadili,anasema mabadiliko ya sayansi n teknolojia yana athari katika mmonyoko wa maadili kama hatuzingatia mambo ya msingi ya kuyachukua kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na kila mtu binafsi.

" Yapo mabadiliko makubwa na yenye athari mbaya kwa sekta zote kwa sasa kutokana  utamaduni wa magharibi na tunahitaji usalama na umakini wa kujua kipi cha msingi cha  kutumia kwa manufaa ya Taifa na mtu binfasi na kipi cha kuacha kutumia" AnasemaTedson 

"Sanaa ya zamani ilikuwa inafundisha maadili kwa wasanii kutunga nyimbo zenye ujumbe,DDC mlimani wana nyimbo inayosema nashukuru wazazi kwa kunilea vizuri,lakini muziki wa wakati huu, utasikia hakuna cha shemeji tunakulaga na ziko nyimbo nyingi zinapotosha maadili tu" Anasema Ngwale

Akihitimisha uwasilishaji wa mada,Mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa Shinyanga,SSP Monica Sahere kupitia mada ya ukubwa wa mmonyoko wa maadili na madhara yake,anasema jeshi la polisi linapokea kwa kasi sana matukio ya ukatili wa kijinsia ya mkoa wa Shinganga.

"Matukio ya ukatili wa kijinsia yanaongezeka kutokana na mmomonyoko wa maadili,mitandao ya jamii  na imani za ushirikina na kufanya watu kulawitiwa,lugha za matusi,kubakwa,kupigwa na wengine  kujinyonga"anasema Monica .

Baadhi ya washiriki wa mdahalo huo wakichangia waliomba serikali kuanzisha mtaala maalum wa maadili kwa shule za msingi kwa sasa kuliko kusubili mdahalo ya ambayo tayari watu wameachwa kuandaliwa toka huko nyuma na kutaka uwepo uthibiti wa mitandao hasa kundi la watu wenye ushawishi kuweka picha chafu mitandaoni wakiwa na kundi kubwa la vijana wanaowafatilia.

MATUKIO MENGINE YA TUKIO

Wanafunzi wakitoa burudani kwa washiriki.

Wasichana wa chuo cha sayansi za afya kolandoto,akizungumzia juu ya  lugha chafu za walezi na wazazi majumbani.

Watumishi wa chuo cha sayansi za afya kolandoto wakisilikiza mada za mmomonyoko wa maadili  nchini.


Baadhi ya Wananchi wa kolandoto walioshiriki katika mdahalo wa mmomyoko wa maadili nchini.
Kaimu Mganga  Mkuu wa chuo cha sayansi za afya kolandoto akizungumzia umuhimu wa vijana kuwa jasiri na kuthamini tamaduni za kiafrika kuliko za mataifa ya magharibi.



Wanafunzi kwa idara zao wakipiga picha na meza kuu.




Ibada ya maombi ya kuombea hali ya mmomonyoko wa maadili chini.



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464