JESHI LA POLISI SHINYANGA LAAGIZA SUNGUSUNGU KUFICHUA WANOHUSIKA NA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI.
Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Mboni Mhita akizungumza na hadhira iliyoshiriki mashindano ya polisi cup wilaya ya Kahama.
Na mwandishi wetu.
JESHI la polisi mkoani Shinyanga limewataka viongozi wa jeshi la Jadi maarufu Sungusungu kuhakikisha linawafichua wazazi na walezi ambao wana waozesha wanafunzi wenye umri mdogo kwa lengo la kujipatia mali.
Maagizo hayo yametolewa na Kamishina Msaidizi wa polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi wakati wa uzinduzi wa mashindano ya polisi Cup wilaya ya Kahama mashindano yaliyo anishwa kwa lengo la kutoa elimu katika jamii juu ya umuhimu wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa kushirikiana na wananchi katika kufichukua vitendo vya uharifu vinavyofanyika katika jamii, iliyofanyika kata ya majengo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.
Magomi amesema kuwa ushirikishwaji wa jeshi la jadi katika kupambana na vitendo vya uhalifu na ukatili wa kijinsia umeshanza katika wilaya zote za mkoa wa Shinyanga ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wananchi kutojichukulia sheria mkononi wakati vitendo hivyo vikifanyika katika maeneo yao na badala yake watoe taarifa ndani ya mamlaka husika kwa hatua zaidi za kisheria.
“ Mkiwa katika kazi ya kupambana na vitendo hivyo vya uhalifu na ukatili wa kijinsia mhakikishe mnashirikiana na jeshi la polisi ili kuepuka kujichukulia maamzi wakati mnapowabaini wahalifu kwenye maendeo yenu ”,amesema Magomi.
Pia Kamanda Magomi amewataka wafanyabiashara pamoja na Makampuni ya ulinzi kuajiri walinzi waliopitia mafunzo nasio kuajiri wazee na walinzi wasio kuwa na sifa.
‘’Anasema, kitendo cha kuajiri wazee katika malindo ni kuepuka gharama ambazo hazina msingi huku wakisahau mali wanazomiliki ni za gharama kwani walinzi hao hulinda kwa kutumia virungu ambavyo haviwezi kuwa msaada kwao pale tukio la uvamizi linapotokea" Anasema Magomi
Awali Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita akiwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya polisi cup wilaya ya Kahama amesema, suala la ulinzi na usalama ni jukumu la kila mmoja ambapo ametumia fulsa hiyo kuwapongeza jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kuwashirikisha wananchi na jeshi la jadi katika kupambana uharifu katika kila hatua hususani vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimeibuka kwa kasi kulinganisha na mtukio mengine.
Hata hivyo Mhita ameyataja matukio yaliyokithiri katika wilaya hiyo kuwa ni pamoja na mauaji yanayotokana na wivu wa mapenzi, Ubakaji, Ulawiti, ndoa za utotoni ambapo amewataka washiriki wa kampeni ya kupinga vitendo vya uhalifu na ukatili kila moja katika eneo lake kuhakikisha anakuwa balozi wa kupambana na vitendo hiyo ili kuvikomesha visiendelee kuwepo.
“ Mboni amesema, jeshi la jadi lina nafasi kubwa katika jamii ya kukemea matukio ya uharifu kwani wao pia wanasauti kubwa na wanaaminika na jamii inayowazunguka, kitendo alichokifanya Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi cha kuwaunganisha jeshi la polisi, wananchi na Sungusungy katika masuala ya ulinzi na usalama kitasaidia kupunguza matukio ya uharifu “Anasema Mboni.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi mkazi wa majengo, Hamis Juma amesema, awali walikuwa wanaogopa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa kuogopa pale watakapojulikana wanatengwa na watu wanaowazunguka,lakini kwa hamasa waliyopewa imewaondolea uoga huo na wako tayari kushirikiana na polisi katika kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ndoa za utotoni kwa wanafunzi zinazokatisha ndoto zao.
Nao baadhi ya Sungusungu walio fika katika uwanja wa Taifa kahama kushudia uzinduzi wa mashindano hayo wameahidi kuendelea kutoa taarifa na kuwafichua wahalifu wanao onekana kwa katika maeneo yao.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464