JUMUIYA YA WAZAZI CCM SHINYANGA MJINI YAFANYA ZIARA KITANGILI

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko na viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini na kamati ya utekelezaji wakitembelea na kukagua ujenzi wa daraja la Kitangili. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini imefanya ziara katika kata ya Kitangili na kukagua ujenzi wa mradi wa Daraja, kutoa msaada Chakula kwa watoto wenye ulemavu wa viungo na akili wanaolelewa katika Kituo cha Brothers of Charity na kuzungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Kitangili.

Ziara hiyo ya Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga walioambatana na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo imefanyika leo Ijumaa Mei 12,2023.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko amesema ziara hiyo pia imelenga kutoa shukrani kwa wanachama wa CCM kufuatia uchaguzi wa ndani ya CCM uliofanyika mwaka jana.

“Tunaendelea na ziara ya kuzitembelea kata zote zilizopo katika wilaya ya Shinyanga Mjini tukihamasisha wanachama na viongozi wa CCM kuipenda CCM na kupinga makundi katika chama ili kuwe na mshikamano kwani mshikamano ndiyo unajenga chama”,amesema Mrindoko.

Mwenyekiti huyo pia amekemea matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na mmonyoko wa maadili unaochangia kuwepo kwa matukio ya ubakaji na ulawiti ambapo amewataka wazazi na walezi kupiga vita vitendo viovu ukiwemo ushoga.

Aidha ametaka hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa watu wanaobainika kufanya vitendo viovu katika jamii.
Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini na kamati ya utekelezaji wakiwasili katika kata ya Kitangili kwa ajili ya kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili.

Katika hatua nyingine ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo.

“Katika ziara hii tumeshuhudia miradi ya maendeleo inaendelea kutekelezwa mfano hata hili daraja linalounganisha kata ya Ibinzamata na Kitangiri ujenzi wake unaendelea vizuri na tunatarajia hadi ifikapo Juni 1,2023 daraja hili ambalo limekuwa kero kwa muda mrefu litaanza kutumika”,amesema Mrindoko.

“Ujenzi wa daraja la Kitangili unaridhisha na mwezi Juni wananchi wataanza kupita pale. Mradi huu unaendelea vizuri”,amesema.
Muonekano ujenzi wa daraja la Kitangili Ijumaa Mei 12,2023.

Akizungumza wakati wa kukabidhi chakula kwa watoto wenye ulemavu wa akili wanaolelewa katika Kituo cha Brothers of Charity, Mrindoko amesema ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anawasaidia watoto hao wenye uhitaji.

“Tunawashukuru walezi wa watoto hawa. Hii kazi mnayofanya kulea na kuwafundisha watoto hawa mambo mbalimbali kwakweli kazi hii mnayofanya ni kazi ya kitume. Tunawashukuru na tunawapongeza sana. Nimeambiwa watoto hawa wenye usonji walikuwa hawajui chochote lakini mmewafundisha jinsi ya kujitambua na sasa wanafanya wao wenyewe. Asanteni sana nasi tunaendelea kukitangaza kituo hiki lakini pia tutaendelea kufika hapa ili tushirikiane kutatua changamoto zinazojitokeza”,amesema.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga

Kwa upande Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi amewataka wanaCCM kuacha viongozi waliopo madarakani kuanzia ngazi ya serikali za mitaa, madiwani na mbunge waachwe wafanye kazi na wapewe ushirikiano wa kutosha.

“Viongozi waliopo madarakani waachwe wafanye kazi kwa sababu muda wa kugombea bado haujafika. Tuwape amani viongozi waliopo madarakani na tunaendelea kukemea makundi ndani ya chama yanayotokana na chaguzi zilizopita”,amesema Kibabi.

Kibabi ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wanachama wa CCM kuendelea kulipa ada za uanachama, kujisajili kwenye mfumo wa kielektroniki, kuongeza wanachama wapya pamoja na kubuni na kuanzisha miradi ili kujiimarisha kiuchumi.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kutoka Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa mbali na kuhamasisha amewataka wazazi na walezi kuepuka mazingira yanayochangia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto ikiwemo kuwalaza chumba kimoja na wageni.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kitangili Mariam Nyangaka amesema utekelezaji wa ujenzi wa madaraja unaendelea vizuri na pindi yatakookamilika wananchi wataondokana na kero ya muda mrefu kwani madaraja yamekuwa kero kubwa kwa wananchi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (kulia) akizungumza wakati viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini  na kamati ya utekelezaji wakitembelea na kukagua ujenzi wa daraja la Kitangili leo Ijumaa Mei 12,2023. Picha na Kadama Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko na viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini na kamati ya utekelezaji wakitembelea na kukagua ujenzi wa daraja la Kitangili leo Ijumaa Mei 12,2023. 
Muonekano ujenzi wa daraja la Kitangili leo Ijumaa Mei 12,2023. 
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza katika daraja la Kitangili Mjini Shinyanga
Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini na kamati ya utekelezaji wakitembelea na kukagua ujenzi wa daraja la Kitangili leo Ijumaa Mei 12,2023. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Sehemu ya chakula kilichotolewa na Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Katibu wa Mbunge Jimbo la Shinyanga Mjini Samwel Jackson akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kutoka Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe Wiswa akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kitangili Zawia Hassan Mpanda akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM kata ya Kitangili
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kitangili Gabriel Swila akisoma taarifa ya kazi za jumuiya ya wazazi kata ya Kitangili kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Shinyanga Mjini

Diwani wa kata ya Kitangili Mariam Nyangaka akizungumza kwenye kikao hicho.
Viongozi wa CCM wakipiga picha ya kumbukumbu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464