Na Abel Michael, Shinyanga Blog
Bonanza la michezo limefanyika leo Mei 20 ,2023 kwenye viwanja
vya michezo vya chuo cha ualimu Shinyanga (SHY COM), kwa kucheza mpira
wa miguu, kati ya timu ya Isamilo Jogging kutoka Jijini Mwanza na
Polisi Jamii Fitness Center kutoka mkoani Shinyanga .
Akizungumza kwenye Bonanza hilo Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa
Shinyanga ACP Janeth Magomi amezitaka Klabu zinazo fanya mazoezi
mkoani humo kuendelea kupinga vitendo vya ukatili na uhalifu katika
maeneo yao ya mazoezi.
Kamanda Magomi amesema kuwa iwapo jamii itashirikiana na jeshi la
polisi katika mapambano ya kupinga vitendo vya ukatili na uhalifu,
itasaidia mkoa wa Shinyanga na Taifa kuwa salama
“Bonanza hili limeshirikisha timu ya PJFC kutoka Shinyanga na Timu ya
Isamilo Jogging kutoka mkoani Mwanza na jeshi la polisi, ili
kuwauganisha kuwa kitu kimoja katika Mapambano dhidi ya vitendo vya
uhalifu na ukatili ndani ya mkoa huo,”amesema Magomi.
Naye Mwenyekiti wa Clabu ya Mazoezi PJFC mkoa wa Shinyanga Sadick
Kibila, amempongeza kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP
Janeth Magomi kwa kujitoa kukilea kikundi hicho na kushiriki katika
mazoezi hali ambayo inawapa motisha ya kuendelea kufanya mazoezi na
kushiriki katika mapambano ya kupinga vitendo vya ukatili na uhalifu
mkoani humo.
Pia Kibila amewashukuru Isamilo Jogging Club kutoka mkoani Mwanza kwa
kufika mkoani humo na kushirikiana nao wakati wa kufanya mazoezi ya
pamoja katika uwanja wa chuo cha ualimu Shinyanga (Shy Com).
Kwa`upande wake mwenyekiti wa Isamilo Jogging Club Abdulrazak Twaha
amewashukuru Clabu ya Mazoezi PJFC kwa mapokezi na ushirikiano mzuri
walio uonyesha wakati wa mapokezi yao
Kamanda Janeth Magomi akikimbia pamoja na wana Jogging.
Wana Jogging PJFC pamoja na Isamilo Jogging Club.
Baadhi ya polisi wakishiriki mbio za Jogging.
Wana Jogging PJFC pamoja na Isamilo Jogging Club.
Baadhi ya polisi wakishiriki mbio za Jogging.
Picha ya pamoja ACP. Janeth Magomi na Timu za mpira wa miguu Isamilo Jogging Club na PJFC
Picha ya pamoja kamanda wa polisi Shinyanga ACP. Janeth Magomi akiwa na wana Isamilo Jogging Club.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP. Janeth Magomi akizungumza na wana Jogging
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP. Janeth Magomi kushoto akikabidhi tuzo ya pongezi kwa aliyekuwa muanzilishi wa Shinyanga Madini Marathoni Roland Mwalyambi ikipokelewa kwa niaba .
Mwenyekiti wa Isamilo Jogging Club Abdurazak Twaha akizungumza na wana jogging.
Timu ya mpira wa miguu PJFC.