KITUO CHA KULEA WATOTO WENYE ULEMAVU CHA ST.JUSTIN CHAPATA MSAADA WA DOLA 10,000 KUTOKA SHIRIKA LA NVEP KWA UFADHILI WA BARRICK

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara,Apolinary Lyambiko (kushoto) akimkabidhi msaada wa hundi ya dola 10,000 Msimamizi wa Kituo kituo cha Kulea Watoto wenye Ulemavu cha St.Justin kilichopo mjini Musoma, Sista Juliana Kitela,katika hafla iliyofanyika kituoni hapo mwishoni mwa wiki. Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow.
Watoto wenye ulemavu wanaolelewa katika kituo cha Kulea Watoto wenye Ulemavu cha St.Justin kilichopo mjini Musoma,walezi wao na wafanyakazi wa kituo hicho wakifurahi baada ya kukabidhiwa msaada wa hundi ya dola 10,000 kutoka kwa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara ,Apolinary Lyambiko,katika hafla ilifanyika kituoni hapo mwishoni mwa wiki. Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko, akiongea wakati wa hafla hiyo.
Msimamizi wa Kituo kituo cha Kulea Watoto wenye Ulemavu cha St. Justin Sista Juliana Kitela akiongea wakati wa hafla hiyo
Mwanzilishi wa Kituo hicho, Sista Magreth John akiongea wakati wa hafla hiyo
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara,Apolinary Lyambiko akipokelewa kwa furaha na watoto alipowasili kituoni hapo.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha St.Justin wakionyesha umahiri wa kucheza ngoma wakati wa hafla hiyo.
Shirika la ya Nos Vies en Partage Foundation (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick,wametoa msaada wa dola za kimarekani 10,000 kwa kituo cha Kulea Watoto wenye Ulemavu cha St.Justin, kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara kwa ajili ya kuimarisha huduma za malezi na kuwajengea watoto hao uwezo wa kujitegemea katika jamii.


Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake,watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.


Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika kituo hicho ,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara,Apolinary Lyambiko, alisema kuwa kila robo ya mwaka NVEP ina utaratibu wa kuelekeza misaada katika masuala yanayolenga kuleta tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii zenye uhitaji, na kwamba hadi sasa limeshasaidia mashirika 12 nchini Tanzania.


Aliongeza kusema kuwa Shirika hili [NVEP] linajikita kutafuta fedha ili kusaidia makundi maalumu katika jamii kama vile wanawake, watoto na mengine yenye uhitaji wa ukuaji wa kiuchumi,


“Leo tunakabidhi msaada wa Dola 10,000 katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu cha St. Justin kupitia NVEP. Kituo hiki ni sehemu muhimu ya jamii yetu, kimeonesha kuwathamini watoto hawa kwa jinsi walivyo bila kuwabagua kwa rangi, dini au kabila,” alisema Lyambiko.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Kituo hicho, Sista Juliana Kitela, ameishukuru Kampuni ya Barrick, akisema msaada huo utapunguza changamoto zikiwemo za kitengo cha jiko katika kituo hicho, ili kuimarisha huduma za malezi na kuwajengea watoto hao uwezo wa kujitegemea katika jamii.


Sista Juliana. amebainisha kuwa Kituo cha St. Justin kinalea watoto wenye ulemavu wa viungo, mtindio wa akili na wasiosikia kwa kuwapatia huduma maalumu na muhimu, zikiwemo za chakula, malazi, matibabu, elimu na mafunzo ya useremala na ushonaji.


Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya watoto wenzake wanaolelewa katika hicho, Ernest Mwita, ambaye ni mlemavu wa akili alishukuru Barrick kwa kujitoa kuwasaidia ili waweze kuwa katika mazingira bora ya kuishi na kupata maarifa.


Kituo cha Kulea Watoto wenye Ulemavu cha St. Justin, kilianzishwa mwaka 2006 na kinaendeshwa na Shirika la Masista Moyo Safi wa Maria Afrika wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma.Kwa sasa kituo hiki kina wafanyakazi 25 na kinahudumia watoto 110, ambapo 75 wanaishi kituoni na 35 wanaishi kwa wazazi na walezi wao nje ya kituo.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464