MADIWANI NA WATENDAJI WATAKIWA KUTOA ELIMU YA MAADILI KWA WATOTO




Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani

Suzy Luhende, Shinyanga blog

Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amewataka madiwani na watendaji wa kata katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, kufundisha maadili mema kwa watoto kwa kuwatembelee mashuleni na kuwapa elimu, ili waweze kuwa na maadili mema.

Hayo ameyasema leo Mei 3,2023 wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani la manispaa ya Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa hiyo, ambapo amesema watoto wanatakiwa kupewa elimu ya maadili na wazazi wanatakiwa kukumbushwa kuzungumza na watoto wao juu ya kufundisha maadili mema.

"Kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii zetu, tunatakiwa tufundishe watoto na wazazi wafundishe watoto wao, ili waweze kuwa na maadili mema tusipofanya hivi tutapoteza nguvu kazi ya Taifa letu,"amesema Meya Masumbuko.

Amesema kila mmoja atoe elimu kwa kila mtoto na mzazi asimame imara kwa mtoto wake, kwani kila mmoja asiposimama imara watoto wa kike hawataolewa na watoto wa kiume hawataowa, hivyo nijukumu la kila mmoja kufundisha watoto na kukemea mambo ya ushoga na usagaji.

Pia Meya amelitaka jeshi la polisi kata kutoa elimu ya usalama kwa jeshi la sungusungu, kwani limekuwa likifanya kazi zake bila utaratibu unaotakiwa, hali ambayo imekuwa ikisababisha migogoro mikubwa katika jamii.

Aidha Meya amesema sungusungu wote wa manispaa ya Shinyanga wanatakiwa kupewa elimu ya usalama kwa sababu wamelalamikiwa kuwa wanafanya kazi zao kinyume na taratibu, hivyo wanajikuta wanaingia kwenye makosa ambayo wamekuwa wakiwaadhibu vibaya wananchi.

"Nawaombeni polisi kata muwasaidie hawa sungusungu muwape elimu ya kutosha ili migogoro isiendelee kutokea katika jamii, kwani sungusungu wamekuwa wakifanya kazi zao bila kuzingatia utaratibu, hawawajui wenyeviti wa vijiji watendaji na madiwani ,hivyo wamekuwa wakiamua jambo wao wenyewe bila ya utaratibu unaotakiwa ,"amesema Meya Masumbuko.

Diwani wa kata ya Ibadakuli Msabila Malale amesema kwenye kata yake tayari ameshakaa na kuzungumza na jeshi la sungusungu kwa ajili ya kufuata utaratibu wa kazi zao, na wameelewa hivyo elimu iendelee kutolewa tu kwa ajili ya kuwakumbusha kufuata utaratibu

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa manispaa hiyo John Tesha ambaye pia ni afisa maendeleo wa manispaa hiyo, amesema jeshi la sungusungu lipo kisheria, lakini linatakiwa lipewe elimu ili liweze kuzingatia taratibu za kazi linazotakiwa kuzifanya,ili lisifanye kinyume na taratibu zake, ambazo zimekuwa zikisababisha migogoro kwa jamii,pia ameahidi kuyatekeleza maagizo yote ya madiwani yanayohusu maendeleo mbalimbali ya kata zote za manispaa.
Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga Ester Makune akizungumza kwenye kikao cha baraza laadiwani
Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga John Tesha akijibu hoja za madiwani
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Anold Makombe akizungumza
Diwani wa kata ya Mwamalili akizingumza kwenye kikao cha baraza
Diwani viti maalumu Manispaa ya Shinyanga akifuatilia taarifabalbali

Diwani wa kata ya Ndala akisoma taarifa ya kata yake
Diwani viti Maalumu Picca Chogelo akihoji jambo
Diwani wa kata ya Chibe akieleza mafanikio ya kata yake
Diwani viti maalumu Sheila Mshandete akielezea mafanikio mbalimbali


Diwani viti maalumu Zuhura Waziri akifuatilia taarifa mbalimbali
Diwani wa kata ya Kolandoto akielezea jambo
Diwani wa kata ya Ndembezi akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya kata yake
Diwani wa kata ya Kitangili akiwasilisha jambo
Diwani wa kata ya KabarageHassan Mwendapole akizungumza
Diwani wa kata ya Mwawaza Juma Nkwabi akiuliza jambo
Diwani wa kata ya Masekelo Piter Koliba akiwasilisha taarifa ya kata yake
Diwani wa kataya Ibadakuli akizungumza
Afisa wa Manispaa akisoma changamoto mbalimbali zilizopo kwenye kata mbalimbali manispaa hiyo
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464