Na Shinyanga
Press Club Blog
Mkutano
mkuu wa umoja wa vyama vikuu vya ushirika vya Pamba Tanzania (TANCOPS) umemsimamisha
na kumuondoa kwenye nafasi ya ujumbe kwenye Ushirika huo Mwenyekiti wa chama
kikuu cha ushirika cha mkoa wa Simiyu (SIMCU) Lazaro Walwa kwa madai ya
kusaliti ushirika.
Hatua hiyo
imejadiliwa na wajumbe wa Mkutano huo na kufikia uamuzi wa kumsimamisha baada ya kukiuka makubaliano ya kuuza
pamba kilo moja kwa Sh 1060 na siyo 1057.
Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mbogwe Mkoa wa Geita Elias Madata,amesema wajumbe wamejadili suala la nidhamu na bei ya pamba na kukubaliana kuandamana hadi ofisi ya Waziri wa Kilimo kumtaka atoe ufafanuzi juu ya baadhi ya tozo zenye ukakasi kwenye ununuzi wa zao la pamba.
Katika kikao hicho wajumbe wameukataa mfumo wa ununuzi wa zao la pamba unaojulikana kama Simiyu modo pamoja na kulalamikia tozo zenye ukakasi wakati wa ununuzi wa zao la pamba.
Naye
Mwenyekiti wa Umoja wa vyama Vikuu vya Ushirika wa Pamba Tanzania Zainab Mahenge,amesema hatua hiyo inalenga
kuwasaidia wakulima wasipunjwe kwa kusainishwa mikataba ya Sh 1057 kinyume na
makubaliano .
Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika wa Pamba Tanzania Zainab Mahenge akizungumzia suala la kuchukuwa hatua ili kuwasaidia wakulima kuuza kwa bei waliyokubaliana.
Mjumbe wa Bodi ya TANCOPS Yahaya Ramadhani akichangia hoja kwenye mkutano
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464