MLINZI AMUWA WAZIRI WA KAZI NA AJIRA KWA KUCHELEWESHA MSHAHARA


Na mwandishi wetu.

Waziri wa Kazi, Ajira na Uhusiano wa Viwanda Nchini Uganda, Charles Okello Engola ameuawa asubuhi hii kwa kupigwa risasi na Mlinzi wake (Bodyguard), Spika wa Bunge la Uganda Anitha Among amethibitisha Bungeni leo.

Tukio hilo limetokea asubuhi hii ambapo imeripotiwa kuwa Waziri Okello alikuwa anatoka nyumbani kwenda kazini ambapo ghafla Mlinzi wake alimpiga risasi kisha akaanza kupiga risasi juu huku akikimbiakimbia Mtaani, Majirani wamesema Mlinzi huyo alisikika akisema hajalipwa mshahara kwa muda mrefu licha ya kufanya kazi na Waziri huyo.

Inaripotiwa kuwa Mlinzi huyo baadaye aliingia Saluni moja iliyopo Jirani na nyumba ya Waziri kisha akawataka waliokuwa ndani kutoka nje na akajifungia na kujipiga risasi na kufariki pia.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464