Picha siyo halisi.
Yeye anakabiliwa na maisha magumu, hali ambayo ilifikia hatua kuwatelekeza watoto wake kutokana na kushindwa kuwa hudumia.Lakini wadau wa kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, (Wanawake Laki Moja) waliwasaidia watoto wa mama huyo katika malezi, kwa kushirikiana na Serikali Ofisi ya Ustawi wa jamii wilayani Kahama huku wakimtafuta Mama yao mzazi.Baada ya kumpata Mama huyo katika kikao kilichofanyika cha wadau wa kupinga ukatili na Ofisi ya Ustawi wa jamii wilayani Kahama, pamoja na Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi, walikubaliana mama huyo arejeshewe watoto wake endapo atakuwa na mazingira salama ikiwamo na mahali pa kuishi.Msaada.Mama huyo kwa sasa anahitaji kupatiwa nyumba ya kupanga yenye chumba kimoja na Sebule, Chakula, Magodoro mawili,pamoja na Mtaji wa kuanzisha biashara ndogondogo ili apate fedha za kuendesha kuhudumia familia yake.kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Anascholastica Ndagiwe ambaye ndiye anachangisha fedha hizo na unaweza tuma pesa kupitia namba yake 0627307579 jina Anascholastica Ndagiwe.Mungu akubariki kwa ulipotoa na akuzidhishie zaidi.AMINA.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464