POLISI SHINYANGA YAKAMATA MADEREVA 932 KWA UKIUKWAJI SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa ACP Janeth S. Magomi
Na Mwandishi wetu.
JESHI la polisi mkoani
Shinyanga limewakamata madereva 932 kwa madai ya makosa ya uvunjifu wa sheria
za usalama barabarani katika kipindi cha mwezi mmoja kupitia oparesheni ya kukamata maderava wanaokiuka sheria za usalama barabarani.
Kamanda wa jeshi la
polisi mkoani hapa ACP Janeth S. Magomi,ameleza hayo leo mei 25,2023 katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Kamanda Magomi amesema katika opareshi hiyo wamehakikisha kuthibiti matukio hatarishi
yanayosababisha ajali za mara kwa mara na kufanikiwa kukamata Magari 944 yaliyokiuka sheria za usalama barabarani hasa makosa ya
mwendokasi.
“Madereva 11 wa kampuni mbalimbali za mabasi ya kubeba
abiria wamefikishwa mahakamani kwa mwendokasi kati ya 90kph na 99kph na maderva
932 walikamatwa kwa kutumia speed radar na VTS wakiwa kwenye mwendokasi kati ya
80kph na 89kph na kuandikiwa faini.”amesema Magomi.
Jeshi la polisi pia limekamata gari mbili aina
ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T202BTW na T358DKM kwa kosa la kughushi nyaraka
za serikali kitendo ambacho ki kinyume
na sheria.
Kamanda Magomi amesema wamefanikiwa kukamata mirungi bando 24, bangi kete 206, viti vya plastiki vinne ,vigae box 8,betri za mnara ya simu02,pikipiki
05,mahine za kurandia mbao mbili,redio tatu na ng’ombe 13,TV-nane,baiskeli mbili ,vifaa vya
kupigia ramli,mbao nane,pampu ya maji moja ,mabati 19,vipande vya chuma saba na
msumeno mmoja .
Aidha,Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limetoa wito wa wananchi
kufuata sheria za nchi na kutojihusisha na vitendo vya uhalifu.
“Jeshi limewataka madereva kutii na kuheshimu alama,michoro na sheria za barabarani wakati wote
na halitosita kumchukulia mtu au kikundi cha watu hatua kali za kisheria kwa
yeyote atakae jihusisha na vitendo vya uhalifu”Anasema magomi.