SERIKALI IANZISHE MTAALA WA MAADILI SHULE ZA MSINGI NA KUWAKAGUA MAAFISA WALIOPATA AJIRA KABLA YA KUAJILI KAMA MAJESHI YANAVYOFANYA.
Wananchi wa kolandoto walishiriki katika mdahalo wa mmonyoko wa maadili nchini.
Na mwandishi wetu.
Serikali imeombwa kuanzisha mtaala maalum kwa shule za msingi nchini ili kuweza kukabiliana na hali ya kuporomoka kwa maadili hapa nchini na kuepuka athari hasi mbalimbali zinazoweza kuathiri serikali na jamii yote.
Hayo yameelezwa leo Mei 13,2023 na Afisa Maendeleo Mkoa wa Shinyanga.Bw Tedson Ngwale wakati akiwasilisha maoni yake katika mdahalo wa kujadili hali ya kuporomoka kwa maadili nchini,uliofanyika katika chuo cha sayansi ya afya kolandoto.
Ngwale anasema,Serikali inapaswa kuanda mtaala maalum kwa kushughulikia hali ya maadili kwa shule za msingi na sekondari ili kuweza kuandaa watoto mapema kuliko kusubili majukwa warsha na makongamano,ambapo ni sehemu wengi hayawafiki na kuwagusa kwa muda muafa hasa kundi la watoto na bado changamoto iko kwa wazazi kushidwa kutimiza wajibu vema kwa malezi na makuzi ya watoto.
Hata hivyo Ngwale,anasema hali ya maendeo na tamaa binafsi imefanya jamii kuthamini vitu kuliko utu wa binadamu na kuwafanya watu kushawishiwa na kutumia miili yao vibaya ili wapate vitu si kujali tena utu wao.
"Naomba kupitia jukwa hili la mdahalo na mbele ya vyombo vya habari ni kuishauri serikali kuchukua hatua ya makusudi ya kuanda mtaala utakao husika moja kwa moja ja watoto wa shule za msingi na sekondari ili kuweza kuthibiti hali ya kuporomoka kwa maadili kwa kuwa wazazi na walezi wanapelea katika wajibu wao kwa maendeleo yaliyopo kwa sasa"anasema Ngwale
Pia Ngwale anasema,ni vema serikali ikaweka hatua ya kuwapima waombaji wote wa ajira serikalini kama inavyofanya katika majeshi yake ili kuzuia kuwa na viongozi wenye tabia ya ajabu kuingia serikalini.
" Serikali ni vema ichukue hatua ya kuanza kukagua maafisa wanaopata ajira kabla ya kuwajili kama majeshi yanavyofanya kwa ajira mpya zinazo tolewa na serikali ili kuthibiti tusije kuwa na viongozi huko badaye wenye kuongoza na kupitisha maamuzi yenye mlengo wa maadili machafu kwa kuwa hawakudhibitiwa tangu mapema" anasema Ngwale.
Kwa upande wake ,Mkufunzi Idara ya Maabara ya chuo cha sayansi za afya kolandoto-Bw Mkama Charles anasema,ni vema serikali kuweka sera ya kuthibiti watu maarufu na mashuhuri wanaoweweka tabia zao za picha za nusu uchi mitandao na kuhamasisha vijana kuwa na tabia mbaya.
"Serikali ichukue hatua ya kuthibiti hizi tabia za magharibi ikiwa nchi za wenzetu kama Korea na China wanaweza na hapa kwetu ni kuamua tu"anasema Mkama
Naye Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho,Paschal Lubadanja anasema ,wazazi wanapaswa kuwa na muda wa kutosha kwa ajili ya kuzunguzma na watoto wao na dawati la jinsia mkoa wa Shinyangan liwe na utaratibu wa kutoa elimu kwa wazazi na walezi ngazi ya kata na mitaa.
Wanafunzi wa chuo cha sayasi za afya kolandoto wakishangia mada ya mmomonyoko wa maadili nchini
Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Shinyanga akizungumza kuhusu namna ya malezi na makuzi yanavyoweza kuathiri mmomonyoko wa maadili.Mwenyekiti wa makundi Maalum SIMAUJATA-Taifa, Bi,Sophia Kang'ombe akizungumzia juu ya namna saikolojia ya tabia inayoathiri mmomonyoko wa maadili.Kaimu Mkuu wa Chuo cha Sayansi za afya kolandoto-Michael Henerco akizungumzia kuhusu usalama wa watoto mashuleni