JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI YAWATAKA WAZAZI KUFUNDISHA WATOTO MAADILI MEMA

Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi CCM wilaya ya ya Shinyanga Fue Mrindoko akipokea taarifa kutoka kwa Katibu wa Jumuiya ya wazazi Kolandoto Sheka Ngusa 

Suzy Luhende, Shinyanga Blog

Kamati ya utekelezaji ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga mjini imewataka wazazi kuwafundisha maadili mema watoto wao ili wasijiingize kwenye vitendo vya ushoga,usagaji, kwani wazazi wengi wamekuwa wakikimbilia kwenye Vikoba shughuli mbalimbali na kusahau kuwapa malezi bora watoto wao.

Agizo hilo limetolewa leo na wajumbe wa kamati hiyo wakati wakiwa kwenye ziara ya kukagua uhai wa Jumuiya ya wazazi katika kata ya Ibadakuli na Kolandoto wilaya ya Shinyanga mjini, kwa ajili ya kuhamasisha wanachama wapya, kuanzisha miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wajumbe kwa kuwachagua.

Mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Shinyanga Fue Mrindoko amesema kuwa kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii, hivyo wazazi wote wasikae na kujisahau kuwaelimisha watoto wakae na watoto wao wazungumze nao mara kwa mara, ili kuwaepusha na janga hilo.

"Ndugu zangu niwaombe sana msijisahau kukaa na watoto wenu kwani kuna watu wanaingia nchini kuja kuharibu watoto wetu wa kiume na wakike kufundisha maadili yasiyofaa, hivyo tunatakiwa tukemee tabia hii ili watoto wetu waweze kupona na janga hili, "amesema Mwenyekiti.

Pia kuna watoto wanafanyiwa ukatili wa kubakwa, kulawitiwa lakini wazazi hawatoi ushirikiano wanafumbia macho baada ya kuelewana na waharifu, hivyo wazazi wanaofanya hivyo tukibaini mtoto amefanyiwa ukatili halafu mzazi hatoi ushirikiano tutamchukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine,"

Kwa upande wake katibu wa jumuiya ya wazazi Shinyanga mjini Dorisi Kibabi amesema vitendo vya usagaji na ushoga vimekuwa vikishamiri sana katika jamii, hivyo watoto wanatakiwa kupewa elimu wakiwa bado wadogo,ili wanapokuwa wanakuwa wanajua kuwa kufanya vitendo hivyo ni kosa.

"Ili watoto wetu wasiendelee kufanyiwa ukatili ni vizuri tunapopata wageni, wajomba, baba wadogo tusiwalaze chumba kimoja na watoto wetu, kuwaepusha wasifanyiwe mabaya maana kesi nyingi za ubakaji ulawiti ni za ndugu kwa ndugu ndiyo maana kesi nyingi zinafumbiwa macho na kumalizwa kimya kimya,"amesema Kibabi.

Pia Kibabi amewataka viongozi wa jumuia ya wazazi kata kuongeza wanachama wapya na kusajiliwa, ikiwa ni pamoja na kubuni miradi mbalimbali kufuga kuku, kulima mazao ya biashara kama alizeti ili kuondokana na kuombaomba pindi wanapokuwa na jambo lao la kijumuia.

Nao baadhi ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya wilaya James Jumbe, amesema kazi ya wazazi ni kuona watoto wanaendelea vizuri katika makuzi na kuwa na maadili mema, hivyo wazazi wanatakiwa wawafanye marafiki watoto wao ili waweze kuwaambia kila wanachokutana nacho,ambapo mzazi atamwelewesha mtoto kuwa kufanya hivi ni kosa.

Kamati ya utekelezaji ikiongozwa na mwenyekiti wake Fue Mrindoko imetembelea kata mbili Ibadakuli na Kolandoto, ambapo kesho itaendelea kutembelea kata zingine ili kuhakikisha inahamasisha uhai wa jumuia hiyo na kukemea vitendo vya uovu katika jamii.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Shinyanga Dorisi Kibabi aakizungumza kwenye kikao cha Jumuia ya Wazazi katika kata ya Kolandoto
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Fue Mrindoko akizungumza na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake katika kata ya Ibadakuli 
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini Janes Jumbe akizungumza kwenye kikao cha CCM kata ya Kolandoto ambapo amewataka wazazi kuwa na urafiki na watoto wao
Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake wakiwa kwenye kikao katika kata ya Ibadakuli 
Katibu wa jumuiya ya Wazazi kata ya Kolandoto Sheka Ngusa akisoma taarifa ya kata hiyo

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini Doris Kibabi akizungumza na wanachama wa CCM na Jumuia zake katika kata ya Ibadakuli ambapo amewataka kuanzisha miradi mbalimbali ili kujiepusha na kuombaomba
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini Doris Kibabi akizungumza kwenye kikao hicho ambapo amewataka wazazi na walezi kuwafundisha maadili mema ili wasijiingize kwenye vitendo vya uovu
Diwani viti maalumu wilaya ya Shinyanga Zuhura Waziri akiwaasa kina mama kulea watoto wao katika maadili mema
Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji Daniel Kapaya akiwaomba wazazi kuchangia Chakula mashuleni ili wanapokula na kushiba waweze kuelewa masomo wanayofundishwa darasani
Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji Joseph Ntabindi akiwaasa wazazi kukaa na walimu wao vizuri wanaofundisha watoto wao
Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Zulfa Hassan ambaye aliwahamasisha viongozi kuongeza wanachama na waweze kujisajili katika Jumuia hiyo
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mary Makamba amewaomba wanachama wote kufanya kazi zao kwa kushirikiana kwa pamoja na waweze kupendana ili kuweza kufanya mambo makubwa zaidi katika Jumuia hiyo

Diwani wa kata ya Ibadakuli Malale Msabila akizungumza kwenye kikao hicho
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Kolandoto Shija Kamuga akizungumza kwenye kikao hicho
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi kata ya Ibadakuli Anthony Makwaiya akizungumza kwenye kikao hicho
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ibadakuli akizungumza kwenye kikao hicho
Katibu muenezi wa chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ibadakuli Amosi Gombo akisoma taarifa kwaniaba ya Katibu wa Jumuiya hiyo

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Kolandoto wakiwa kwenye kikao hicho wakisikiliza kamati ya utekelezaji jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwaasa

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Kolandoto wakiwa kwenye kikao hicho wakisikiliza kamati ya utekelezaji jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwaasa

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Kolandoto wakiwa kwenye kikao hicho wakisikiliza kamati ya utekelezaji jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwaasa
























































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464