TAKUKURU YABAINI MIANYA YA RUSHWA KATIKA MFUMO WA UTOAJI MBOLEA NA UENDESHAJI WA MASOKO -SHINYANGA.
Na mwandishi wetu.
Takukuru mkoa wa
Shinyanga yabaini mapungufu na uwepo wa mianya ya rushwa katika mfumo wa utoaji wa pembejeo katika wilaya ya kahama na mfumo wa
uendeshaji wa masoko katika wilaya ya Kishapu.Takukuru imebani dosari
hizo baadaya kufanya uchambuzi wa mifumo kwa halmashauri za hizo kwa kipindi cha januari hadi machi 2023.
Mkuu wa Takukuru Mkoa
wa Shinyanga,Donasian Kessy ameeleza hayo leo mei 25,2023 katika vyombo vya
habari mkoani shianyanga,wakati akiwasilisha taarifa ya robo ya tatu ya mwaka
wa fedha 2022/2023(Januari hadi machi 2023) juu ya uthibiti wa vitendo vya rushwa
mkoani shinyanga.
Kessy anasema,Takukuru
ilifanya uchambuzi wa mifumo katika halmashauiri ya wilaya ya Kahama na Kishapu
ili kuweza kuziba mianya ya rushwa ,ambapo walibaini mapungufu katika utoaji wa
pembejeo kwa kata zongomera,busoka na mwendakulima za wilaya ya Kahama na dosari ya uendeshaji wa soko la maganzo
wilaya ya Kishapu.
“Vitabu vya usajili havirudishwi kwa wakati vituoni,kwani wakulima bado
wanahitaji kujiandikisha na hata waliojiandikisha hawapati mrejesho wowote au
namna ya siri ili kwenda kuchukua mbolea na baadhi ya wakulima kusajiliwa Zaidi
ya mara moja kwenye mfumo wa kuandaliwa namba ya siri tofauti ,mfano kijiji cha
zongomela baadhi ya wakulima waliandikishwa mara mbili”anasema Kessy
“kukosekana
kwa rejesta inayoonesha idadi ya wafanyabiashara kwa kila soko na rejesta ya
fremu zinazozunguka soko la maganzo” Anasema kessy.
Kwa upande mwingine,Takukuru walipokea malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya taasisi ndogo za fedha
kukataa kutoa salio la deni analodaiwa mteja pindi anapoomba salio la deni
lake.
“Malalamiko mengi yalihusu benki ya ABC tawi la Kahama ambapo ofisi
iliingilia kati na benki hiyo kutoa taarifa za salio la deni kwa wahusika”anasema
kessy
Katika hatua
nyingine,Takukuru ilifatilia miradi ya maendeleo arobaini na nne(44) yenye
thamani ya Tshs bilion 5.1 na kubaini
mapungufu katika miradi miwili(2) yenye thamani ya tshs million 86 ambapo mradi
wa vyumba viwili vya madarasa katika sekondari
ya bunambiyu wenye thamani ya tshs million 40 na ujenzi wa madarasa mawili yenye thamani ya
tshs milioni 46 ya shule ya sekondari ikonda.
“Katika shule ya sekondari bunambiyu,jengo kutosimikwa vizuri kwenye
kuta pamoja na dari,kopo za madirisha kupinda,madirisha ya aluminium kutokwekwa
vizuri na badaya yake kukandikwa na sementi nyeupe,kuwepo na nyufa kwenye
baadhi ya madirisha na mikanda ya bodi kuachia nyufa”
“Kwa upande wa
shule ya sekondari ikonda,mzabuni alilipwa tshs million 5 tangu julai 2022 na
hakuwahi kupelekea vifaa vya ujenzi”anasema kessy.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464