Na Mwandishi wetu.
Shinyanga
ZAHANATI ya Kijiji Cha Bugogo kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga iliyodaiwa kufungwa baada ya Mganga aliyekuwepo kufariki Sasa imefunguliwa na kuletwa mwingine ambaye ameanza kutoa huduma Dk. Simoni Wilson
Zahanati hiyo ilikuwa na watumishi wawili ambapo muuguzi pekee ndiye aliyebaki na kuelemewa na utoaji wa huduma zote ikiwemo uzalishaji wa wajawazito na huduma za kliniki kwa watoto takribani zaidi ya miezi sita.
Wakiongea na HABARILEO leo baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho akiwemo Diana Tungu alisema Zahanati hiyo imefunguliwa na kuanza kutoa huduma na mganga ameanza kufanya kazi.
"Tulikuwa tunakwenda kituo cha afya Samuye umbali wa kilomita 15 kupata huduma hata Kijiji jirani cha Mwamala ni mbali tumeteseka hasa wajawazito na watoto"alisema Tungu.
Muuguzi Lenny Kinkoro alisema alipata changamoto kubwa kuwa peke yake kwenye utoaji wa huduma kwa Wagonjwa takribani Wagonjwa 20 kwa siku na wajawazito wanaojifungua takribani 12 kwa siku na huduma za kliniki kwa watoto.
"Kupatikana mganga imekuwa nafuu kwani wakati mwingine Wagonjwa wengine ninawaacha kwenda kutoa huduma za mkoba Kijiji Cha Bunonga ambacho hakina Zahanati kabisa" amesema Kinkoro.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Bugogo Seleli Mabula alisema Mganga wameanza kumuona jana akifanya kazi Sasa wamefika watumishi wawili hawatoshi aliomba Serikali iongeze wengine angalau wawe watumishi wanne.
Diwani wa kata hiyo Hamis Masanja alisema kata hiyo ina vijiji vinne ambavyo ni Bugogo,Bunonga,Mwamala na Ibanza ikiwa Kuna jumla ya wakazi zaidi ya 12,000.
"Kijiji Cha Bunonga kina wakazi zaidi ya 4000 hakina Zahanati na Kijiji Cha Bugogo kina watu zaidi ya 3000 na wote wanategemea huduma kutoka kwenye Zahanati hii"alisema Masanja..
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464