WAANDISHI WA HABARI WAFUNDWA NA TAMWA KATIKA KULINDA USALAMA WAO



Waandishi wa habari kutoka mikoa mitano wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na TAMWA

Suzy Luhende, Shinyanga blog

Chama cha waandishi wa habari Wanawake (TAMWA) Kimetoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mikoa mitano ya Kigoma,Shinyanga,Singida, Tabora na  Simiyu lengo
 kuwajengea uwezo wa ulinzi na usalama pale wanapotimiza majukumu ya kazi zao.

Akitoa ufafanuzi wa mafunzo hayo meneja mradi na mikakati kutoka TAMWA Silyvia Daulinge leo Mei 24,2023 amesema hayo mkoani Tabora nakueleza wameandaa mafunzo ili kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa na Ulinzi na usalama wakati wa kufanya kazi zao.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Edwin Soko amesema vipo vitisho mbalimbali wamekuwa wakifanyiwa waandishi wa habari kunyimwa taarifa kutukanwa, hivyo mafunzo hayo yatasaidia kukabiliana na hali hiyo ili kuweza kupungua au kuondoka kabisa madhira yanayowakuba waandishi na waweze kufanya kazi zao kwa uhuru.

Soko amesema waandishi wa habari wanaandika habari nyingi na kusababisha serikali kufahamu na wadau kuibua ajenda,lakini waandishi wanatakiwa kufanya kazi zao huku wakijua usalama wao upo katika eneo salama.

Soko amesema kuna ulinzi wa aina mbili kuna phyisical Security na Digital Security hivyo vyote vimekuwa vikitokea kwa waandishi wa habari na takwimu za kidunia waandishi 57 waliuwawa, 65 walishtakiwa ,533 wamefungwa na 49 walipotea katika maisha ya kutatanisha.

"Baraza la habari Tanzania (MCT) kwa takwimu walizozitoa mwaka 2022 waandishi wa habari 18 walinyanyaswa,walitishiwa na wengine kunyimwa taarifa"amesema Soko.

"Tunataka kabla mwandishi hajaenda sehemu fulani kufanya kazi tujue kuna usalama, atajikinga vipi ili kupunguza madhira,anaweza kwenda kwenye shughuli mbalimbali za kisiasa tujue huko kuna usalama, tunajipanga mapema "amesema Soko.

Soko amesema ofisi za waandishi wa habari zinatakiwa ziwe na usalama wakutosha na vitabu vya kuwaandika wageni wanaokuja kuwatembelea wafahamike kwa ulinzi wa waandishi sio waingie tu hivyo waige kama ofisi zingine.

Baadhi ya waandishi wa habari Fednad Irunde kutoka Singida na Kareny Masasy wamesema hali ya vyombo vya habari ni mbaya sana kwani bado waandishi wa habari wanapata vitisho.

"Viongozi wa serikali wanaoteuliwa wanatakiwa kuelimishwa,kwani waandishi wamekuwa wakiandika habari za kweli katika jamii,lakini viongozi hao wanakimbilia kuwatishia maisha kuwapeleka mahakamani" Ramadhani Rajabu kutoka Singida

Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Suzy Butondo amesema waandishi wengi wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kutishwa pale wanapofanya kazi zao, kunyimwa taarifa mbalimbali, lakini hawaripoti ili kuondokana na changamoto hiyo kila mwandishi atoe taarifa ili baadhi ya watu ama viongozi  wanaowafanyia vitisho, kutukana waandishi waache

Meneja mradi na mikakati kutoka TAMWA Silyvia Daulinge akitoa maelekezo kwenye mafunzo ya waandishi wa habari


Edwin Soko akitoa elimu ya masuala ya ulinzi na usalama wa waandishi wa habari
Waandishi wa habari kutoka mikoa mitano wakimsikiliza mwezeshaji wa mafunzo hayo Edwin Soko
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya masuala ya ulinzi na usalama wa waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya masuala ya ulinzi na usalama wa waandishi wa habari


Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya masuala ya ulinzi na usalama wa waandishi wa habari

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya masuala ya ulinzi na usalama wa waandishi wa habari

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya masuala ya ulinzi na usalama wa waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya masuala ya ulinzi na usalama wa waandishi wa habari
Meneja mradi na mikakati kutoka TAMWA Silyvia Daulinge akitoa maelekezo kwenye mafunzo ya waandishi wa habari kutoka mikoa mitano







Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464